Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akisalimiana na Maseneta
kutoka Ufaransa waliomtembelea Ofisini kwake Luthuli katika jiji la Dar
es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiskiliza kwa makini
wakati alipokutana na Maseneta kutoka Ufaransa waliotembelea Ofisini
kwake Luthuli jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kiongozi wa Maseneta
hao Senator Hervé Maurey.

Sehemu ya Maseneta kutoka
Ufaransa waliomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano
na Mazingira Mh. Mussa Zungu Ofisni kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es
Salaam. Maseneta hao wako Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiwa katika picha ya
pamoja na Maseneta kutoka Ufaransa waliomtembeleaOfisini kwake mtaa wa
Luthuli jijini Dar es Salaam. Alichoshika mkononi ni medali aliyopewa na
Maseneta hao.
………………………………………
Serikali ya Tanzania imeahidi
kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala yote yanayohusu mazingira
na Serikali ya Ufaransa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Mh. Mussa Zungu wakati alipokutana na Maseneta kutoka
Ufaransa waliomtembelea katika Ofisi yake ndogo iliyopo Luthuli jijini
Dar es Salaam.
“Tanzania inapenda kushirikiana
na Ufaransa kwenye masuala ya mazingira wala msiwe na hofu wala
kigugumizi kuanzia leo tutataandaa maeneo ya vipaumbele ya kushirikiana
nyinyi na sisi na tuweze kufanya kazi kwa pamoja” alisitiza Waziri
Zungu.
Akijibu swali la Seneta mmojawapo
aliyeuliza kuhusu suala la ukataji miti kwa Tanzania, Waziri Zungu
alisema kuwa anawahakikishia Maseneta hao kuwa kwa sasa hakuna tena
kuharibu mazingira ikiwepo suala la ukataji miti kwa sababu Wizara
inasimamia suala la mazingira ipasavyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la
Hifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC) akiongea katika Mkutano huo
amesisitiza kuhusu uwekezaji wa nishati mbadala ili kuweza kumkomboa
Mwananchi wa kawaida kabisa aliyepo kijijini pia akasema kuhusu suala la
kupatiwa teknolojia ya urejelezaji taka.
Maseneta hao wameshukuru kwa
ukarimu waliopatiwa wakati wa ziara yao Nchini Tanzania na kuishukuru
Serikali ya Tanzania kwa ukarimu huo na kuahidi kushirkiana nao kwa
dhati kabisa katika kutatua changamoto mbalimbali za mazingira kwa
pamoja. Maseneta hao sita kutoka Nchini Ufaransa wako Nchini Tanzania
kwa ziara ya kikazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...