Meya wa Washington DC, Muriel Bowser huko Marekani usiku wa kuamkia leo ametangaza hali ya hatari katika mji huo baada ya kuenea wimbi la maambukizi ya virusi hatari vya corona.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, wakuu wa jiji la Washington DC wametangaza hali ya hatari katika jiji hilo na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu wanaozidi elfu moja.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi za maafisa wa afya wa Marekani, hadi hivi sasa zaidi ya watu elfu moja na mia moja wameambukizwa virusi vya corona nchini humo na watu wasiopungua 31 wameshafariki dunia.

Hivi sasa wananchi wa Marekani wanamshutumu vikali rais wa nchi hiyo Donald Trump kwa kudharau wimbi hilo la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo. Trump ameonesha madharau makubwa kuhusu wimbi hilo na amesema ataendelea na kampeni zake za uchaguzi kama kawaida bila ya kushughulishwa na virusi vya corona.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...