Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akisisitiza kuwasilisha orodha ya
majina ya wataalamu wa kufundisha Kiswahili kwa wageni kwa Waziri wa
Mambo ya nje kwa lengo la kusambazwa katika balozi mbalimbali Tanzania
nje ya nchi leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya kuimarisha
stadi za kufundisha
Kiswahili kwa wageni kwa wahadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma yaliyoratibiwa na Baraza la Kiswahili Tanzania.
Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la
Kiswahili Tanzania Consolata Mushi akitoa taarifa kwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuwa taasisi
yake tayari imekwisha sajili jumla ya wahitimu 1224 katika kanzidata ya
wataalamu wa mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wageni,leo jijini Dodoma
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa wahadhiri wa Kiswahili katika
chuo kikuu cha Dodoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dodoma Prof.Justine Ntalikwa akimweleza Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe leo Jijini
Dodoma kuwa jumla ya wahadhiri ishirini na moja wanaofundisha lugha ya
Kiswahili katika chuo hicho
wanashiriki mafunzo hayo kwa ya stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni yatakayofanyika chuoni hapo kwa siku nne.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma wahadhiri wa lugha ya
Kiswahili watakaoshiriki mafunzo kwa kuimarisha stadi za kufundisha
lugha ya Kiswahili kwa wageni,mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo leo
Jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki- WHUSM, Dodoma
Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Stadi
za kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni ambayo yanatolewa kwa
wahadhiri 21 wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Mheshimiwa Mwakyembe alisema kuwa fursa za kufundisha lugha ya
Kiswahili duniani ni nyingi, hivyo watanzania wanapaswa kujitokeza kwa
wingi kutumia fursa hizo katika kujiongezea kipato pamoja na kukuza
lugha hiyo.
“Serikali iliona uhitaji wa waalimu wakufundisha lugha ya
Kiswahili nje ya nchi ,hivyo iliamua kuanzisha kanzidata ya wataalamu
hao ambao kwa sasa wamefikia 1,224 na nchi mbalimbali zimeanza kutuma
maombi ya uhitaji wa wataalam hao” alisema Mhe.Makyembe.
Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa orodha ya majina ya wataalam wa
lugha hiyo itawasilishwa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki na Balozi za Tanzania nje ya nchi kwa lengo la kurahisisha
upatikanaji wa wataalamu hao.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili
Tanzania (BAKITA) Bibi. Consolatha Mushi alisema kuwa mafunzo hayo
hutolewa kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu katika taaluma ya lugha ya Kiswahili
kuanzia Shahada ya kwanza hadi Uzamivu.
“Mafunzo haya yanatolewa na BAKITA ikiwa ni kutekeleza agizo
ulilolitoa wewe Mhe.Waziri Agosti mwaka 2018 wakati ulipotembelea Baraza
letu na kubaini kuwa hakuna takwimu halisi za wataalamu wa lugha ya
Kiswahili nchini hivyo Baraza limetekeleza agizo hilo” alisema
Bibi.Consolatha.
Ameongeza kuwa hadi sasa mafunzo yameshatolewa kwa mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga Mwanza na Arusha lengo kiwa ni
kuwaanda waalimu wa Kiswahili kunufaika na fursa mbalimbali za Kiswahili
zinazojitokeza ndani na nje ya nchi.
Naye, Dkt.Samweli Mgaya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma Idara
Kuu ya Kiswahili, alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wataalamu hao
kueneza lugha adhimu na aushi ya kiswahili kwa namna ambavyo inatakiwa
hasa matumizi sahihi ya lugha hiyo.
Mafunzo haya yameanza kutolewa machi 9 hadi machi 13,2020 kwa
ushirikiano Ndaki ya Insia na Elimu na Jamii pamoja na Idara ya
Kiswahili, ikiwa ni awamu ya pili kutolewa hapa Jijini Dodoma baada ya
awamu ya kwanza kufanyika mwezi Oktoba, 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...