Gharama za maisha kwa wakazi wa kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoani Tanga, zimetajwa kupungua kutokana na uwepo wa umeme jua unaozalishwa na kusambazwaa na kampuni ya Ensol
Wakizungumza na Michuzi Blog,wakazi hao wamesema awali iliwalazimu kutumia mafuta ya taa ambayo yaligharimu shilingi kwa siku, hali ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma kimaendeleo.
Aidha wamesema licha ya nishati hiyo kuwapunguzia gharama za maisha pia imekuwa chachu ya wao kujikwamua kiuchumi kama ilivyo kwa mzee Mussa Mkande ambaye ni mfanyabiashara wa duka.
Mkande amesema sasa analazimika kufunga duka sa nne usiku badala ya saa 12 jioni, kutokana na kuwepo mwanga wa umeme unaoimarisha usalama.
Aidha amebainisha kuwa umeme huo umemsaidia kuongeza pato lake la siku kwa kuuza shiling elfu 70 au 80, ambapo hapo awali alikuwa akipata shiling elfu 50 na hii ni kutokana na uuzaji wa vinywaji vilivyphifadhiwa katika jokofu.
Mbali na hilo wanakijiji cha mpale pia kwa sasa hawapitwii na habari au matukio mbalimbali,kwani mzee Mkande ameweka banda la kuangalia televisheni kwa kingilio cha sh 300 hadi 500 na nyakati za mpira huwatoza shilingi 1000, hali ambayo pia inamuongezea kipato.
Lakini si mzee Mkande tuu hata Vijana wa kijiji hicho wamejiongezea kipato kwa kuendesha bodaboda ambazo wana uwezo wa kujaza upepo kijijini hapo kwa kupitia mmoja wa wakazi kumiliki Mtambo wa kujaza upepo ambao awali huduma hiyo haikupatikana.
Si uendeshaji wa bodaboda tuu Bali hata saluni zinapatikana sasa kijijini Mpale na hii ni kutokana na uwepo wa umeme unaorahisisha kazi za vinyozi na kuwaigizia kipato vijana waliojiajiri kwa njia ya saloon.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...