Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania
kutotishwa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya
Corona (Covid-19)
na badala yake waendelee kuchapa kazi na kujenga uchumi huku wakizingatia
tahadhari zote za kujikinga kuambukizwa ugonjwa huo kama zilivyotolewa na
wataalamu.
Mhe. Rais Magufuli
amesema hayo leo tarehe 22 Machi, 2020 alipohudhuria Ibada ya Jumapili katika
Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma,
iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Onesmo Wisi.
Katika salamu zake
katika Ibada hiyo, Mhe. Rais Magufuli amesema kuwepo kwa ugonjwa wa Corona
isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mwenyezi Mungu, hivyo ametoa wito
kwa Wakristo na Waumini wa madhehebu mengine kumrudia Mwenyezi Mungu ili
aepusha janga hili, badala ya kumwacha shetani atawale.
Mhe. Rais Magufuli
amekemea tabia za baadhi ya watu wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huu ama
kuwatia hofu wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na
badala yake ametaka Watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakizingatia
tahadhari.
“Watu tusitishane, tunatishana
mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu
ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee
kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa
ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza
uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Amewashukuru
viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi
kuchukua tahadhari na ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa
ili Mwenyezi Mungu aepushe balaa hili la Corona.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
22 Machi,
2020
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejumuika
pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la
Dodoma katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Onesmo
Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na
badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari
zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejumuika
pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la
Dodoma katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Onesmo
Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na
badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari
zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana amani na
waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma
bila kushikana mikono katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa
hilo Padre Onesmo Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na
ugonjwa Corona na badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku
wakizingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini
wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma na Watanzania
katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Onesmo
Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na
badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari
zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti
Takatifu, alipoungana na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa
Msalaba Jimbo kuu la Dodoma katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa
kanisa hilo Padre Onesmo Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania
kutotishwa na ugonjwa Corona na badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi
huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Padre
Onesmo Wiss wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma bila
kushikana mikono wakati wa ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko huyo,
ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na badala
yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari zote za
kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
Waumini nje ya Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma mara
baada ya ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Onesmo
Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na
badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari
zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...