Baadhi ya washarika wakiwa wanatawanyika mara baada ya ibada ya kwanza katika KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok
Naibu Katibu mkuu  Misioni na Uinjilisti Dayosisi kaskazini Kati Jackson Kahembu akinawa mikono mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kwanza kama anavyoonekana katika picha.

Baadhi ya washarika wakiwa wanatawanyika mara baada ya ibada ya kwanza katika KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok

Baadhi ya washarika wakiwa mara baada ya kumalizika kwa  ibada ya kwanza (hawakusalimiana kama iliyo desturi) katika KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok
Mwinjilist Eliezer Mbasha akinawa mikono(hakuwa zamu leo) KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok,ambapo waumini walilazimika kunawa mikono na kutumia sun
Mmoja wa waumini akinawa mikono kabla ya kuingia ibada ya pili,katika kanisa la Kkkt Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok


Na.Vero Ignatus Arusha.

Wazazi wametakiwa kuwa waangalifu na kuhakikisha kuwa wanapata muda wa kutosha na watoto pamoja na kuwapa elimu namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kwani ugonjwa huo unadhibitika kama watafuata maagizo yaliyotolewa na wizara ya Afya

Hayo yameelezwa na mchungaji kiongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Arusha Mashariki Usharika wa Engarenarok Solomoni Dereva na kuwataka waumini kuzingatia maelekezo ya serikali kama ilivyoelekeza huku wakimuomba Mungu kuwaepusha na gonjwa hilo kwani hakuna jambo linaweza kuwatenga na Upendo wa Mungu katika hali yoyote ile.


Amesema wamelazimika kusitisha  Shule ya jumapili kwa Watoto,darasa
la Kipaimara,badala yake wainjilisti wataandaa masomo na kuwapatia wazazi ili
waweze kuwasaidia watoto wao hiyo ni kutokana na changamoto hiyo ya virus vya
Corona

Kwa upande wake Jackson Kahembu Naibu Katibu mkuu Mission na Uinjilisti Dayosisi akihubiri katika ibada ya jumapili kanisani hapo amewasihi waumini hao kujenga Imani kwa Mungu kwani hakuna jambo la kumshinda Mungu,bali anachohitaji kutoka kwao ni Imani pamoja na kukumbuka utoshelevu wa Mungu maishani mwao.


''Hebu kumbukeni habari ya  Kristo alivyoweza kuwalisha watu 4000 kwa kuibariki mikate7 na samaki 5 watu waliokuwa wamekaa nae kwa siku tatu lakini walikula wakashiba na kusaza vikapu 7 kama aliweza kuwalisha hao ni zaidi ya kufanya kila kitu maishani mwetu ikiwa ni kutuondolea kabisa gonjwa hili la corona''!alisema.


Kahembu aliwataka wazazi kuhakikisha watoto wanakula vizuri vyakula vyenye vitamini C pamoja na maji ya kutosha ili kuikinga miili yao na maradhi yanayoweza kuepukika.


 Amekemea tabia ya wazazi wengi kutokufanya kile ambacho serikali imeagiza juu ya watoto kukaa majumba badala yake watoto wengi wanazagaa mtaani jambo ambalo siyo sawa,hivyo amewaagiza kila mzazi atenge muda na watoto wao na kuwapa elimu na kuchukua tahadhari juu ya virusi vya Corona

‘’Serikali imefunga shule
kuanzia za awali hadi sekondari ili waweze kukaa nyumbani chini ya uangalizi wa
wazazi ila wazazi wengi hawajatimiza hilo

Aidha kanisani hapo waliweka vifaa vya kunawia mikono kwa asilimia kubwa ambapo viongozi wa kanisa hilo waliweka uangalizi maalumu kuhakikisha kabla ya muumini mmoja mmoja hajaingia kandani ya nyumba ya ibada alinawa mikono kwa sababuni na maji pamoja na suntizer


Kwa wakati tofauti Rais wa Tanzania Mhe.Magufuli amekemea baadhi ya watu wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huo kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii,badala yake amewataka kuendelea kufanyankazi huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo kama zilivyotolewa na wataalam wa afya


Aidha amesema hakuna sababu ya kutishana bali amewaomba Wakristo na waumini wa madhehebu mengine kwamba wakati huu ndiyo mzuri wa kumtegemea Mungu kuliko wakati mwingine wowote,na kusema kuwa hawawezi kusalimu amri kwa ugonjwa huo wa Corona na kuacha kumtegemea Mungu

Mhe.Magufuli amesema kuwa kuanzia kesho march 23,2020 wasafiri wote ikiwemo watanzania takaoingia nchini kutoka katika mataifa yaliyoathirika na ugonjwa wa COVID-19 watafikia sehemu ya kujitenga kwa siku 14 na watakaa huko kwa gharama zao wenyewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...