SERIKALI imesema imepanga kukarabati Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mwadui kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (EP4R).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli wakati alipofanya ziara ya kutembelea shule hiyo na kubaini uchakavu wa miundombinu.

Mweli amesema uchakavu wa miundombinu ndio haswa unaochangia kushindwa kufanya vizuri kwa shule hiyo ambayo awali ilikua ikisifika kwa ubora wa elimu.

Amesema elimu ya ufundi ni muhimu sana kwa watoto haswa katika kipindi hiki ambacho Nchi inaelekea katika Uchumi wa Kati wa Viwanda hivyo ni lazima izalishwe nguvu kazi yenye taaluma ya ufundi itakayosaidia katika viwanda.

' Ujio wangu hapa umelenga kujionea uchakavu wa miundombinu ya majengo ikiwemo katakana hii ambayo sasa haina ubora ule wa mwanzo, hata madarasa ni wazi hayawezi kuleta kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wetu.

Hivyo sisi kama Serikali tunaangalia namna gani tunaweza kuinusuru kwa kufanya ukarabati mkubwa utakaorudisha shule hii kwenye hadhi yake," Amesema Mweli.

Amesema kupitia mradi wa lipa kutokana na matokeo “Ep4r” watakarabati shule hiyo na kuirudisha kwenye hadhi yake ili iendelee kutoa elimu ya ufundi wa watoto wanaochaguliwa katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe Nyabaganga Taraba amesema Majengo mengi ya shule ya Ufundi Mwadui yamechakaa na
mashine nyingi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zimekufa hivyo shule haiwezi kutoa elimu ile iliyokusudiwa hapo awali.

“ Mhe Naibu Katibu Mkuu tunashukuru kwa ujio wako tunaamini Shule hii ikikarabatiwa itakua mkombozi wa watoto wa Kishapu maana watapata ujuzi wa kutosha wa kuweza kuwasaidia katika maisha yao hapo baadae na ninaishukuru Serikali kwa kuona uchakavu uliopo na kuahidi kuikarabati nina uhakika kiwango chetu cha Elimu kitaongezeka baada ya ukarabati huo” Amesema Taraba.

Naye Mkuu wa Shule ya Ufundi Mwadui amesema shule hiyo ilijengwa mwaka 1961 kwa ufadhili wa Mgodi wa Almasi wa Williamson na kwa  sasa ina wanafunzi 800; Elimu ya ufundi inayotolewa kwa sasa ni ujenzi, useremala, umeme na kuchonga  vyuma.
 Muonekano wa baadhi ya majengo ya Sekondari ya Ufundi Mwadui ambayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli ameitembelea.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli akikagua madawati na madarasa katika shule ya Sekondari ya Ufundi Mwadui.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli akitoa maelekezo baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya shule ya sekondari ya ufundi Mwadui.
 Naibu Katibu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anaeshughulikia elimu, Gerald Mweli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mwadui baada ya kumaliza zira yake ya ukaguzi shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...