Charles James, Michuzi TV

MTANDAO wa Watumishi wa Umma Wanawake ujulikanao kama Viongozi Wanawake Wanaochipukia Tanzania’  (EWLT) wamekuja na mpango wa kuleana na kubadilishana uzoefu katika kufikia malengo chanya ya kiuongozi.

Akizungumza katika uzinduzi wa mtandao huo mmoja wa waanzilishi, Bi Glory Mboya kutoka
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) amesema mtandao huo una lengo la kukuza Vijana wakike katika kufikia ngazi za juu za uongozi.

Bi Mboya amesema mtandao huo utajikita zaidi katika kubadilishana uzoefu baina ya viongozi wanaoibuka na viongozi waandamizi wenye uzoefu Serikalini ili kuwajengea kujiamini, kujituma kuwajenga na kuwavutia vijana wa kike wanaotaka kuingia katika Utumishi wa Umma na kujenga utamaduni wa Watumishi wa Umma wanawake kutoa mchango katika kusaidia jamii inayowazunguka.

Katika hafla hiyo, wajumbe wa Mtandao huo walijadili masuala muhimu ya kujitambua na kujithamini katika maeneo ya kazi, kufanya kazi zao kwa kujituma na kuhakikisha wanafikia malengo yaliyowekwa na Taasisi, kuupenda na kuuthamini Utumishi wa Umma,  kuweka uwiano wa maisha ya kazi na maisha binafsi.

Nae hiyo Mwanzilishi mwenza wa mtandao huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa (OR-TAMISEMI), Beatrice Kimoleta amesema bila kuwajengea uwezo vijana wa kike kujiamini na kutambua uwezo wao itakuwa vigumu kwao kufikia nafasi za juu za uongozi.

Aidha, Kimoleta amesema wanawake wengi wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na kushindwa kuweka uwiano katika kumudu au kutekeleza majukumu ya kazi na familia. (Work life Balance).

" Wanawake tunatakiwa kutambua mipaka ya kazi zetu pasipo kuchanganya na maisha binafsi, na tusipofanya hivyo tunakuwa kwenye hatari ya kuathiri kazi na familia.

Tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii kubwa na kwa wakati na kuhakikisha tunafikia malengo ya mwajiri kwa kiwango anachotarajia (There is no compromise on that) na unaporudi nyumbani ufanye majukumu ya kifamilia kwa ufanisi pia,  yaani muda wa kazi fanya kazi na muda wa familia utumikie kwa familia ipasavyo, endapo utachanganya hivi vitu viwili na kushindwa kuweka uwino (balance) utaharibu sehemu zote mbili hali ambayo itakuongezea msongo wa mawazo na kupunguza ufanisi wako," Amesema Kimoleta.

Nae mwanzilishi mwenza ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sakina Mwinyimkuu amesema ili mtumishi mwanamke aweze kufikia malengo katika utumishi wake ni lazima aongozwe na mawazo thabiti na halisi.

" Pia ni lazima tutambue udhaifu wetu na tufahamu vyema jinsi ya kuishi na mapungufu yetu na kuyafanya bora na halisi katika maisha yetu ya kila siku tuwapo kazini na tunapotekeleza majukumu ya familia," Amesema Sakina.

Naye Mratibu wa Mafunzo kutoka Taasisi ya Uongozi ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa wazo hilo, Kanisia Mkwizu amesema kuwa katika kipindi hiki watumishi wanawake wanatakiwa kuzingatia akili hisia  (emotional Inteligence) kwasababu zimekuwa zikiangaliwa  kama kitu muhimu sana kwa viongozi kuweza kumudu majukumu yao kwa ufanisi.
 Watumishi wa Umma Serikalini wenye maono yanayofanana wakiendelea na majadiliano ya Mpango wa Kuibua Viongozi wanawake Serikalini wakati wa hafla yao ya uanzilishwaji wa mtandao wao.
 Watumishi wa Umma  Wanawake ambao wamekutana Jijini Dodoma kujadili Mpango wa kuibua Viongozi Wanawake Serikalini pamoja na kusaidia kufikia malengo yao.
Mwanzilishi mwenza wa Mpango wa Kuibua Viongozi Wanawake Serikalini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa (OR-TAMISEMI), Beatrice Kimoleta akizungumza katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...