WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, amekagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma na kusema kuwa serikali imedhamiria shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka huu kufanyika kwenye jengo hilo jipya la Tume hiyo.


Amebainisha hayo wakati alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya Tume hiyo, leo tarehe 10 Februari, 2020, ambapo amekagua hatua za ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa kukagua Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa .

Kukamilika kwa majengo hayo itakuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambaye aliitaka tume hiyo kuhakikisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo unakamilika kwa wakati, ili shughuli za uchaguzi Mkuu wa mwaka huu zinafanyike kwenye majengo hayo.

Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL ndio wanaohusika na shughuli za ukandarasi wa majengo hayo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga jingo lake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama, akikagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma, leo Februari 10, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akisistiza ekieleza umuhimu wa Jengo Jipya jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma, leo Februari 10, 2020, mara baada ya kukagua hatua ya ujenzi wa Ofisi hizo.


Muonekano wa Jengo la NEC linaloendelea kujengwa jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...