Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu amaeahidi kupeleka Wataalamu wa mazingira  kwa ajiili ya kufanya tathmini  katika eneo la Kwamgogo lililopo Kisiwani Pemba ambalo limeathirika na mabadiliko ya tabianchi. Amesema hayo kisiwani Pemba alipotembelea eneo hilo kujionea athari za kimazingira zilizosababishwa na mabadiliko ya tabinchi. 

Ameongeza kuwa lazima jitihada za haraka zichukuliwe katika eneno hilo ili kuweza kuepusha kisiwa cha Pemba kisiharibiwe na mabadiliko ya tabianchi. “ tutaleta Watu wafanye tahtmini ni kitu gani tufanye ili kuzui haya maji kuja tena au kuyazuia yarudi huko yalikotoka na kuweza kunusuru eneno hili”alisema Waziri Zungu

Kijiji cha Kwamgogo kimeathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kusababisha maji kujaa na kuharibu mazingira ikiwemo kusababisha Wananchi kukosa njia ya kupita wakati wanaenda sokoni au kwenye shughuli zao za kila siku hivyo kusababisha Wananchi kuvuka kwa kuogelea kwenda ng’ambo ya pili kwenye huduma muhimu za kijamii. 

Amewashukuru pia Wananchi wa Mkoa huo na Uongozi wa Mkoa kwa kuweza kuchukua hatua kwa kupanda mikoko na ili kuweza kupunguza athari hizo za kimazingira katika kijiji hiko cha Kwamgogo. “Namshukuru saana Mkuu wa Mkoa pamoja na Wananchi wa eneo hili kwa jitihada mlizofanya kulinda mazingira katika eneo hili” alisema Zungu

Ziara hiyo ya Mheshimiwa Zungu ni maagizo aliyopewa na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi  baada ya kumtembelea Ofisini kwake kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemedi Suleiman wakati alipowasili kisiwani Pemba kwa ajili ya ziara ya siku moja kutembelea eneo la kwa Mgogo lililoharibika na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akielezea jambo wakati wa ziara ya kutembelea kijiji cha Kwamgogo kilichoko kisiwani Pemba ambapo alienda kujionea athari za kimazingira katika kijiji hiko ambazo zimesababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu  akiongea na Wananchi wa kijiji cha Kwamgogo mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kijiji hiko kilichoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali wa Mkoa wa kusini Pemba pamoja na Wananchi na watoto waliohudhuria katika mkutano wake na Wananchi wa kijiji cha Kwamgogo alikofanya ziara kujionea athari za kimazingira zilizosababibishwa na mabadiliko ya tabia Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...