NA VICTOR MASANGU,
PWANI
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani amewataka wanachama wa Chama hicho
kuhakikisha wanachagua wagombea watakaowawakilisha vema katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwenzi Octoba mwaka huu.
Alisema ni vema kuzingatia kumpigia
kura mgombea ambaye wanaamini atakwenda kuwa kielelezo kizuri kwa wananchi
atakaposhindanishwa na wengine kutoka vyama vya upinzani.
Gama alitoa angalizo hilo wakati wa mkutano wa kura za maoni katika kata
ya Tangini Halmashauri ya mji wa Kibaha ambapo Mfaume Kalanguti aliongoza kura
za maoni.
Katibu wa CCM kata ya Tangini Zuhura
Sekelela alisema wamejipanga kata hiyo kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi
Octoba.
" Tunataka Tangini sasa irejee
kuongoza na CCM hatutaki kuwaachia wapinzqni tena, tunachotaka ni ushirikiano
kwa wanachama tupate mwakilishi mzuri na atakayekubalika na wananchi. alisema
Zuhura.
Alisema, ili kuendeleza mshikamano
ni vema wanachama kujenga tabia ya kukubaliana na matokeo ya kura za maoni, na
kuachana na tabia ya kwenda kwenye mikutano wakiwa na matokeo yao mfukoni
changamoto ambayo imekuwa ikisababisha mgawanyo wa wanachama baada ya kura za
maoni.
Akitangaza matokeo ya kura za maoni
kata hiyo, Msimamizi wa uchaguzi Juma Gama alimtaja Mfalme Kalanguti
kuongoza kwa kupata kura 45, akifuatiwa na Philemon Mabuga aliyepata kura 28 na
Alto Yombayomba kura 8.
Katika kata ya Mailimoja Ramadhani
Lutambi aliongoza kura za maoni kwa kupata kura 75 akifuatiwa na Christopher
Mjema kura 45 na Sudy Mohamed kura 8.
Kata ya Mkuza Focus Bundala kura
113, Erneus Mapunda kura 17, Ahmed Masimba kura 6, na katika kata ya Sofu Mussa
Ndomba kura 33, Yusuph Mbonde kura 15 na Barton Mwaki kura 7.
Kata ya Nianjema Bagamoyo Abdul
Pyalla alipata kura 56, Rajabu Swed 51 na Columbas Kayangwa kura 45.
Caption- 1 Pichani Mfaume Kalanguti
ambaye ameibuka kuwa mshindi baada ya kupata kura 45 katika kura za maoni
kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM kwa ajili ya kuwania nafasi ya
udiwani Kata ya Tangini.(Picha na Victor Masangu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...