Na Mwandishi wetu, Babati
Aliyekuwa
mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Mkoa wa Manyara mwaka
2007/2012 Cosmas Bura Masauda ambaye aligombea kura za maoni ya ubunge
wa jimbo la Babati Mjini kisha wajumbe wakampa kura moja amesema yupo
tayari kupeperusha bendera ya CCM pindi jina lake likirudishwa na CCM.
Masauda
akizungumza Julai 27 amesema yupo tayari kupeperusha bendera ya chama
hicho kupitia jimbo la Babati Mjini kwani hatawapa kazi kubwa viongozi
kumuuza kwa wananchi tofauti na wengine.
Masauda
ambaye alisimamishwa uanachama mwaka 2016 na kurudishiwa kadi ya CCM
Julai 14 mwaka huu kisha uchaguzi wa kura za maoni ukafanyika Julai 22
alipata kura moja ya wajumbe.
"Mimi
baadhi ya viongozi walinisimamisha wakidai kuwa sikumuunga mkono
mgombea ubunge wa CCM wa mwaka 2015 Kisyeri Werema Chambiri na madiwani
wa kata tano jambo ambalo siyo la kweli kwani nilikuwa napinga udhalimu,
rushwa na viongozi kuwa na wagombea wao mfukoni mwao," amesema
Masauda.
Amesema
alirudishwa CCM siku ya kuchukua fomu Julai 14 na kwenye uchaguzi Julai
22 akapata kura moja, amewashukuru wajumbe kwani hakufanya kampeni ila
wenzake walianza miaka miwili iliyopita na kuambulia kura tatu, mbili
hadi sifuri.
"Mambo
yaliyofanyika kwa wajumbe kwenye kura ya maoni yanatisha kwani kama huna
pesa usijaribu ubunge ila namwomba Mungu jina lirudi ambalo litakuwa
sahihi kwa wananchi atupe mbunge atakae kubalika na jamii nzima ya
Babati mjini," amesema Masauda.
Amesema
wajumbe siyo kipimo cha kumpata mgombea mbunge kwani wasiokuwa na fedha
waliambuliwa kushangiliwa kwa maelezo na kuambiwa muda, muda, na ana
amini vikao vya juu vitaamua kwa umakini mkubwa mno.
Amesema
viongozi wa CCM wa mkoa wanapaswa kutumia weledi wao katika kung'amua
madhambi yaliyofanyika na kutoa haki kabla ya kwenda ngazi za CCM
Taifa.
"Kuna watu
wanasema hadharani kuwa wameshamaliza kamati kuu ila watambue kuwa
wananchi wana macho na watu wa Babati wana misimamo yao naomba yasije ya
mwaka 2015 yakajirudi, tulipoteza jimbo na madiwani watano nampongeza
Rais Magufuli kwani akigundua jambo hana rafiki ni refa mwenye kadi
nyekundu tuu njano hana nawasikia wananchi wanasema walionunua wajumbe
wakimleta kwao itakula kwao ila wakimleta aliyepita buree na wao tutampa
bure CCM hoyee," amesema.
Amewaomba
wanaotafuta kura hivi sasa ili majina yao yarudishwe waache mpaka Rais
mstaafu wa awamu ya nne Benjamin Mkapa atakapozikwa kwani aliyefariki ni
mtu muungwana aliyekataa malofa kuchukua nchi na msiba huo ni mkubwa
kwani watanzania wapo kwenye ibada katika msiba huu mkubwa.
Amesema
yupo tayari kupitishwa na kusimamishwa kugombea ubunge wa jimbo la
Babati Mjini kwani hatawapa kazi kubwa ya kunadiwa na pia vijana
watampitisha kwa miluzi.
Amesema anajulikana kwa misimamo isiyoyumba katika kupinga rushwa, hana unafiki, amenyooka na fitina kwake ni mwaka.
"Mchakato
wa uchaguzi ulitawaliwa na rushwa yaani vyuma viligongana siyo benki
siyo simu ni kurushiana muamala tuu kwa baadhi ya wagombea na wajumbe na
usiposema sasa kipindi cha Rais Magufuli tutasema lini tena,
tusipozungumza hivi sasa tunaongea kwenye utawala upi?" amehoji
Masauda.
Aliyekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa mwaka
2007/2012 wa Mkoa wa Manyara, Cosmas Bura Masauda akijieleza kwa wajumbe
wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Babati Mji ili kuomba kuchaguliwa
katika kura za maoni kugombea ubunge wa jimbo la Babati Mjini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...