Na Woinde Shizza , Michuzi TV-Arusha
KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Philimon Mollel amewahaidi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya kujenga kiwanda kila kata pindi watakapompa ridhaa ya kupeperusha bendera ya ubunge katika nafasi ya Jimbo la Arusha Mjini
Akizungumza katika mkutano mkuu maalumu wa kupiga kura za maoni za Chama hicho wa kumchagua mgombea atakayesimama kupeperusha bendera ya ubunge,amesema jimbo la Arusha Mjini limekuwa na changamoto ya vijana kukosa ajira, hivyo akipewa ridhaa kiaumbele chake cha kwanza atakachofanya ni kujenga viwanda katika kila kata na hiyo itamsaidia kupunguza tatizo hilo.
Aidha amefafanua Jimbo la Arusha Mjini linahitaji mtu mwenye busara kama yeye ambaye atahakikisha ataleta maendeleo na sio vurugu za kisiasa ambapo zimesababisha baadhi ya miradi kuchelewa
Ameongeza kuwa Rais John Magufuli ameleta miradi kikubwa, hivyo ni wakati wake wa kwenda bungeni kupambania maslai ya wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini kwakua jimbo litakuwa na muwakilishi mwenye uchu wa Maendeleo.
Aidha amesema kuwa katika kuinua maendeleo ya vijana ,wamama na wazee atahakikisha wanapatiwa mikopo ya riba nafuu ili waweze kujiajiri wenyewe ili waweze kuhudumia familia zao.
Akinukuu vitabu takatifu Cha bibilia kutoka methali 29-2 unaosema wenye haki wanapotawala watu wanafurahia lakini mtu muovu anapotawala katika Jimbo watu wanapata shida,watu wanateswa ,watu wanahumia hivyo aliwaomba wananchi wamchague ili aweze kuwapa Raha na kuwaaidi wakimchagua atasukuma Maendeleo na tumbo.
Picha ikionyesha Mgombea ubunge kupitia Chama Cha mapinduzi Philimon Mollel akiomba Kura mbele ya wajumbe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...