Na Woinde Shizza ,Arusha
RICHARD Paul maarufu Marcas ameomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kutokana na utendaji kazi alioufanya katika jamii
Akizungumza wakati wa kuomba kura ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Paul amesema alishawahi kufanya mambo malimbali ikiwemo uanzilishi wa kukusanya mapato ya maegesho ya magari (Parking )Mkoa wa Arusha mbali na kazi hiyo pia kazi ingine aliyoifanya ni pamoja na kushauri Twiga Bank kuwa bank ya Posta mara baada ya kuona bank hiyo kuwa na matawi manne na kukusanyamadeni na baadae kuwa moja ya bank kubwa nchini
Pia amesema ni mkusanyaji wamadeni sugu mamlaka ya usimamizi wa bandari zote Tanzania pamoja na mdai ya madeni sugu ya wanafunzi wa chuo cha bandari
Amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Arusha hatasaidia wakina mama wanao panga bithaa bara barani eneo la frence cona wanapata maeneo ya kufanyia biashara zao mahali salama zaidi
Katika sera yake amehaidi atazungumza na watu wa national housing pamoja na viongozi wa chama na Serikali ili kupata jengo katikati ya mji kwa ajili ya kujenga City market
Amewaomba wajumbe kumpa ridhaa kwani jimbo la Arusha linaitaji mtu mwenye maono kama ya kwakwe aweze kusaidiana na John Magufuli kuendeleza Tanzania ya uchumi wa kati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...