NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Stella Manyanya amepongeza jitihada zinazofanywa na wakulima pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya viwanda katika kuongeza thamani za mazao huku akisisitiza utumiaji wa teknolojia zinaoshauriwa na wataalamu.

Naibu Waziri Manyanya ameyasema hayo alipotembelea Banda la Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika (African Wildlife Foundation-AWF) katika maonesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mashariki, ambapo amewapongeza AWF kwa kuja na Teknolojia ya kukausha zao la Kokoa kwa kutumia sola katika maonesho hayo ili kuwawezesha wakulima kujifunza na kuweza kutumia katika maeneo yao na kupata Kokoa zenye ubora.

 Aidha, amewataka wakulima wa Kokoa Kanda ya Mashariki kutembelea Banda hilo ili kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza thamani na kuzalisha Kokoa zenye ubora ambazo zitaendana na mahitaji ya soka la kimataifa na kuongeza pato la taifa.

Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka AWF Alexander Mpwaga amesema shirika hilo limekuwa likitoa Elimu kwa wakulima kutoka maeneo yote ambayo wanalima Kokoa hapa nchini, huku akiongeza kuwa lengo la kushiriki katika maonesho ya wakulima nanenane ni kutoa elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kuongeza thamani ya zao hilo ikiwemo jinsi ya kuvundika, kukausha na kusindika ili kupata bidhaa iliyo na ubora. 

Vilevile, amesema kuwa shirika la AWF limekuwa likitoa elimu kwa jamii inayowahudumia juu ya kukabiliana na maambukiza ya Covid 19 na athari zinazotokana na ugonjwa huo kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya.

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Stella Manyanya akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mradi kutoka AWF Alexander Mpwaga wakati alipotembelea Banda la AWF Kanda ya Mashariki.
 Banda la kukaushia kokoa (solar drying facility)


Maboksi ya kuvundikia kokoa (cocoa fermentation structures)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...