Mrajisi
wa vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, akizungumza kwenye banda la
Vodacom katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya nanenane,wakati
wa uzinduzi wa mfumo wa M-Kulima unaowawezeaha wakulima kuwasiliana na
kufanya miamala kwa kutumia mtandao wa Vodacom. Pembeni ni naibu
Mrajisi, Charles Malunde na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania PLC Kanda
ya Ziwa, Ayubu Kalufya(kulia).
Mkuu
wa Mauzo Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mfumo wa M-Kulima unaowawezesha wakulima
kuwasiliana na kufanya miamala,mfumo huo umezinduliwa kwenye viwanja vya
Nyakabindi mkoani Simiyu kwenye maonesho ya nanenane, Mrajisi wa vyama
vya Ushirika Dk Benson Ndiege (kushoto) Naibu Mrajisi Charles Malunde.
Wakulima
wakifuatilia hotuba za uzinduzi wa mfumo wa Vodacom M-Kulima
unaowawezesha kufanya miamala na kuwasiliana kwa urahisi, mfumo huo
umezinduliwa kwenye viwanja vya nanenane Nyakabindi mkoani Simiyu.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa katika picha ya pamoja na Mrajisi baada ya uzinduzi wa M-Kulima



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...