Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Matumizi ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mtakuja, Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akifuatilia taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Matumizi ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mtakuja, Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma iliyowasilishwa kwake na kamati maalum iliyoundwa na Serikali.

Mjumbe kutoka kamati maalum ya kushughulia mgogoro wa Mtakuja Ndugu Wincheslaus Kweyunga (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Mtakuja kwa Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mjumbe kutoka kamati ya kushughulia mgogoro wa Mtakuja Ndugu Wincheslaus Kweyunga (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Mtakuja kwa Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi

***************************************

Na: Eliafile Solla

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na kamati maalum iliyokuwa inashughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi Kata ya chang’ombe jijini Dodoma leo Desemba 11,2020 ambapo amepokea taarifa kuhusu mgogoro huo.

Mgogoro wa matumizi ya ardhi wa Mtakuja, Kata ya Chang’ombe katika eneo lenye hekta 10 umedumu kwa muda mrefu licha ya jitihada mbalimbali za Serikali za kuutafutia ufumbuzi.

Serikali iliunda kamati maalum ya kushughulikia mgogoro huo wa matumizi ya ardhi na baadae kuamua kupanga na kupima eneo hilo na kubadilisha matumizi kutoka yale ya awali na kuwa Makazi kutokana na uhalisia na maendelezo yaliyokwisha kufanyika kupitia mradi wa maboresho wa mwaka 2015.

Kamati hiyo imekutana na Mhe. Lukuvi jijini Dodoma leo na kuwasilisha taarifa na mapendekezo yake jinsi ya kuushughulikia mgogoro huo ambapo Mhe. Waziri Lukuvi atatoa maagizo baada ya kuipitia taarifa hiyo na kujiridhisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...