Na Tiganya Vincent, Tabora

FEDHA zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) zimemwezesha mlengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Belita Lutema  kuanzisha mradi wa kuvuna maji ya mvua ambayo kila siku unampatia kipato cha elfu 30.

Mlengwa huyo alitoa ushuda huo jana wakati viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kujifunga mafanikio ya walengwa.

Belita alisema baada ya kupata fedha za TASAF alichimba shimo na kujnga  kisima chenye urefu wa futi 16, kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua ambapo kwa kiwango anachopata pata kwa kila siku anachopata kinamhakikishia kufikisha shilingi milioni 8.1 kwa miezi 9.

Belita alisema kwamba kisima hicho kimekuwa mkombozi kutokana na kumuingizia kipato cha fedha jambo ambalo TASAF imeweza kumsaidia kumuinua kimaisha.

Mlengwa huyo mwenye familia ya watoto 7 ,alisema tangu alipoanza kupata ruzuku hiyo alianza kununua mifugo ya kuku 2. na Mbuzi ndipo alipoweza kuishi vizuri na familia yake.

Aidha Belita aliendelea kusisitiza kwamba amepata mafanikio makubwa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf,jambo ambalo hakutegemea kufikia hatua hiyo kubwa.

Mlengwa huyo alitaja mafanikio aliyoyapata katika awamu zote ni kulima shamba la mahindi ekari 2 ambapo anategemea kuvuna kiasi cha gunia 45 na kwa sasa amekwisha hifadhi magunia 12 mahindi kwa ajili ya kuuza mara baada ya soko kiwa zuri.

Hata hivyo alisema nje ya mafanikio hayo ameweza pia kujenga nyumba bora na kupangisha wapangaji kwa kila mwezi anawatoza shilingi 20.

Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanapata ruzuku kupitia mpango huo kutumia wanazopata katika shughuli za uzalishaji mali kwa  lengo la kujiua kiuchumi na  kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .

Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwawezesha fedha za mpango huo na kufanikiwa kujitegemea na kuilea familia yake ya watoto 7 .

Mlengwa huyo alisema hata akitolewa katika Mpango huo hawezi kushindwa kujimudu yeye na familia yake katika m mahitaji mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...