Meneja wa Maduka ya wa Kampuni ya  Mafuta  ya TOTAL Jane Mwita akizungumza kuhusiana na Siku ya Wapendanao 'Valentine Day' namna walivyojipanga kutoa Upendo kwa wateja wao katika kitoo cha Mafuta cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mteja wa TOTAL Elizabeth Amul akizungumza Mara baada ya kuweka nafuta katika gari kake katika kituo cha mafuta cha Oysterbay ikiwa Total inarudisha upendo kwa wateja wao kwa zawadi.

Elizabeth Amul akifurahi Jambo katika kituo cha mafuta cha TOTAL Tanzania ikiwa ni Siku ya wapendanao alipita kuweka mafuta kituo hicho,jijini Dar es Salaam.
Benjamin Simon akizungumza mara kuweka mafuta katika kituo cha mafuta Oysterbay ikiwa total inarudisha Upendo kwa wateja wao 'Valentine Day'

 KAMPUNI ya Mafuta ya TOTAL na Maduka yake yaliyopo katika  Kituo cha Mafuta cha Oyster bay Barabara ya Alhasan Mwinyi wamerudisha upendo kwa wateja wao kwa zawadi ikiwa ni Siku ya Valentine Day.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kituo cha Mafuta cha Oyster bay Meneja wa Maduka Bonjour TOTAL, Jane Mwita amesema kuwa Februari 14 ni siku ya wapendao ambapo Total inarudisha upendo kwa wateja wao.

Amesema kuwa TOTAL imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kwa Siku kama ya leo kutoa upendo kwa wateja wanaoendelea kutumia bidhaa za TOTAL kuanzia kwenye Mafuta, vilainishi pamoja na bidhaa mbalimbali za Maduka ya TOTAL.

Mwita amesema kuwa wanapromosheni ya ya Dairy Milk kwa sh. 2800 zikiwa mbili ikiwa ni punguzo kutoka sh.4000 kwa mbili.

"Total inathamini wateja wake katika kuonyesha upendo na kuendelea kuthamini kupata huduma za TOTAL hii ndio mchango  wake mteja kwetu na tunahidi kuendelea kutoa huduma bora." Amesema Mwita.

Elizabeth Amuli ni mteja aliyepata huduma ya Mafuta katika kituo cha Mafuta Oasterbay amesema TOTAL wamekuwa na utaratibu mzuri kwa kutukumbuka wateja katika Siku ya wapenda nao.

Amuli amesema Siku ya wapenda nao  'Valentine Day'  watu wanaichukulia tofauti lakini Siku ya kupendana ndani ya jamii pamoja na familia kwa kila mmoja kuonyesha upendo kwa mwenzake.

Na Benjamin Simon amesema yeye ni mtu wa makamo amesema vijana wamekuwa na mawazo ya kufanya Valentine Day ni siku ya starehe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...