Mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Mwadui FC, Timu ya KMC FC kwa mara nyingine itashuka dimbani kesho kumenyana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, KMC ambao ni wenyeji dhidi wapinzani wao Kagera Sugar, utachezwa saa 14:00 mchana ambapo tayari maandalizi ya mwiso yamefanyika na kwamba wachezaji wote wapo kwenye morali nzuri kuelekea kwenye mtanange huo.

Timu ya KMC ambayo ipo chini ya kocha mkuu John Simkoko inahitaji ushindi katika mchezo huo ilikuweka ilikuweza kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.

“ Tunahitaji kushinda mchezo wetu wa kesho, ushindi ni mkakati wetu wa kwanza, tunajua duru hii ni ngumu kwasababu kila timu inahitaji alama tatu muhimu, kikubwa tunaendelea kujituma katika maandalizi yetu kila mchezo kwetu ni fainali lengo ni kuhakikisha kwamba kwenye mchezo huo tunakwenda kupata alama tatu.

Hadi sasa KMC ipo kwenye nafasi ya sita ikiwa na alama 28 na kucheza michezo 20, mbapo Februali 16 ilipata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya mwadui, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...