Charles James, Michuzi TV

SERIKALI na Umoja wa Ulaya, zimetiliana saini ikataba sita ya Msaada wa Euro milioni 111.5 sawa na sh. bilioni 308 kwa ajili ya kutekeleza miradi 6 katika sekta za kilimo, nishati, uboreshaji wa mazingira ya biashara na ushirikiano wa kiufundi..

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya-Tanzania Mhe. Manfredo Fanti, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James lisema kuwa Mradi wa kuboresha Sekta ya Nishati umepatiwa sh. bilioni 96.7 na Mradi wa Matumizi Endelevu ya Nishati ya Kupikia (sh. bil. 82.8), na mradi wa Kusaidia Mnyororo wa Thamani katika Ufugaji Nyuki (Sh. bil.27.6).

Miradi mingine ni mradi wa Kuboresha Huduma ya Afya ya Mimea ili kuongeza usalama wa chakula nchini (bil. 27.6), Mradi wa Kusaidia Kuboresha Mazingira ya Biashara, Ukuaji na Ubunifu (bil. 63.5) na Mradi wa Ushirikiano wa Kitaalamu utakao gharimu sh. bilioni 9.7 na kufanya jumla ya miradi yote kuwa Sh. bilioni 307.9.

“Tangu Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) zianze kushirikiana mwaka 1975, umoja huo umetupatia misaada na mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 7.3 ambapo shilingi trilioni 6.6 ni misaada na kiasi kilichobaki cha sh. bilioni 748.2 ni mikopo yenye masharti nafuu sana ikilinganishwa na ile ya kibiashara” aliongeza Bw. James

Bw. James aliushukuru Umoja wa Ulaya kupitia kwa Balozi wake hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti kwa msaada huo ambao hauna masharti yoyote jambo ambalo linaonesha jinsi Umoja huo ulivyo na mahusiano mazuri na Tanzania kwa muda mrefu.

"Nikiri wazi kwamba Umoja wa Ulaya ni wadau wetu wakubwa wa maendeleo na kupitia misaada hii inayotolewa kupitia Mpango wa Ushirikiano wa 11 kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania, imeeelekezwa kutatua mahitaji na changamoto zilizoainishwa katika mpango ya maendeleo ya kitaifa hususani mpango wa pili wa maendeleo (FYDP II) 2016/17 - 2020/21 na MKUZA II.

Alisema kuwa misaada iliyotolewa imezingatia mahitaji ya nchi na changamoto zilizoainishwa kwenye mipango ya maendeleo ya kitaifa na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliyopangwa ikiwemo kukuza viwanda kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi. .


Bw. James alisema kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP III) ambao uko katika maandalizi pamoja na Dira ya Maendeleo 2050 iliyoidhinishwa hivi karibuni kwa upande wa Zanzibar ni nyenzo muhimu katika uandaaji wa mpango ujao wa ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Umoja huo.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini, Mhe. Manfredo Fanti ameipongeza serikali ya Tanzania kwa namna ambavyo imekua ikitekeleza miradi yote ambayo inashirikiana na Umoja huo jambo ambalo linazidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya pande hizo mbili.

"Ni wazi kwamba mikataba hii ni viashiria vya namna ambavyo Serikali ya Tanzania na EU tumekua tukishirikiana bila vikwazo, tuna furaha kuona kwamba Serikali imekuwa ikitekeleza miradi kwa umakini mkubwa nasi tunaahidi kuendeleza ushirikiano huo” Alisema Mhe. Balozi Fanti.

Alisema anaamini kuwa miradi hiyo sita itakayotekelezwa kupitia msaada huo itaoresha zaidi maisha ya watu hususan katika kipindi hiki cha mapinduzi ya viwanda kwa kuboresha sekta ya nishati, kilimo pamoja na kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotengenezwa nchini zinakuwa salama na kuzingatia ubora wa kimataifa.

“Tanzania haijanufaika sana na soko huru la umoja wa Ulaya kutokana na bidhaa kutozalishwa kwa wingi na kutokidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa katika soko hilo, lakini kupitia miradi huu naamini mnyororo wa thamani wa mazao utaongeza tija na kukuza biashara” alisema Mhe. Manfred

Hafla hiyo ya utiaji saini ilihudhuriwa pia na Wizara zinazonufaika na miradi hiyo akiwemo Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Muipango Zanzibar Bw. Rashid Said Rashidi.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anaye shughulikia Masuala ya Fedha za Nje Bi. Amina Khamisi Shaaban, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye, Kamishna wa Huduma za Misitu Prof. Dos Santos Silayo nnna baadhi ya wakurugenzi na maafisa wa Wizara kutoka Wizara hizo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakionyesha mikataba mara baada ya Serikali kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akipongezana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakisaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma Katika ni Mwanasheria wa Wizara ya Fedha Bi.Loveness Msechu akishuhudia.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James ,akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka wizara mbalimbali wakifatilia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ,akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 kwa Kuipa Tanzania fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdeo ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.Amina Shaaban ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James ,akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...