Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi ameongoza wananchi mbalimbali wanaoishi FCkatika Kata ya Lwanwima kupanda miti ya maparachichi katika Shule ya Msingi Lwanwima ikiwa ni sehemu ya kampeni ya wilaya hiyo kuzifanya shule zote za kijani.

Kulingana na maelezo ya Afisa Misitu wa wilaya hiyo, Deogratius Julius, kampeni hiyo inalenga kupanda miti katika shule za sekondari na msingi na hata katika maeneo ya taasisi za umma.

Hadi sasa wameshapanda miti 41,996 katika kipindi hiki cha mvua.

Wadau mbalimbali wa mazingira walishiriki zoezi hilo wakiwemo Aga Khan Healrh Services kupitia mradi wake wa Impact kanda ya ziwa ambao walikabidhi miche 280 ya maembe na maparachichi

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt.Philis Nyimbi akipanda mti wa mparachichi ikiwa ni kampeni ya wilaya hiyo kwa Shule za ,Msingi na Sekondari.

Picha mbalimbali katika kampeni ya upandaji miti ya miparachichi katika wilaya ya Nyamagana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...