RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo Katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza kuhusiana na  ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Aboubakar Kunenge amesema ziara hiyo itaanza Jumatano ya Februari, 24 ambapo Rais Dkt. Magufuli atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwaajili ya uzinduzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

Aidha RC Kunenge amesema siku ya Alhamis ya Februari 25 Rais Dkt. Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 Asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambako kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.

RC Kunenge amesema siku ya Ijumaa ya Februari 26, Mhe. Rais atafanya shughuli ya uzinduzi wa Nyumba za  Polisi na Kiwanda cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika Saa 03:30 asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...