Afisa Sheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw.
Zephania Lyamuya akizungumza katika kikao cha kusuluhisha mgogoro wa
kurudiwa wimbo uitwao “Mungu Baba” wa Bi. Upendo Nkone uliorudiwa na
Studio ya Dom -Tune bila ridhaa ya msanii huyo katika kikao kilichofanyika
katika Ofisi za Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma.Kulia kwakwe ni msanii wa
muziki wa Injili Bi. Upendo Nkone.

Mlezi wa Dom-Tune studio Askofu Damasi Silivesta(wa kwanza kulia)
wa Kanisa la THE WORLD MINISTRY akifafanua jambo wakati wa kikao cha
kusuluhisha mgogoro wa kurudiwa wimbo uitwao “Mungu Baba” wa Bi.
Upendo Nkone uliorudiwa na Studio hiyo bila ridhaa ya msanii huyo katika
kikao kilichofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma,Kulia kwake
ni watayarishaji wa muziki wa Studio hiyo Bw. Kassim Ali na Samweli Yona.

Na Shamimu Nyaki - WHUSM, Dodoma
TAASISI
ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kimetoa agizo kwa wadau wa kazi za
Sanaa kuacha kurudia kazi za msanii bila ridhaa au makubaliano na
mmiliki wa kazi hiyo.
Wito
huo umetolewa leo Feburari 11, 2021 Jijini Dodoma na Afisa Sheria wa
Taasisi hiyo Bw. Zephania Lyamuya alipomaliza kusuluhisha mgogoro wa
kurudiwa wimbo uitwao “Mungu Baba” wa Bi. Upendo Nkone uliorudiwa na
Studio ya Dom -Tune bila ridhaa ya msanii huyo.
Akizungumza
katika kikao hicho Afisa Sheria huyo amesema kazi yoyote ambayo
imesajiliwa katika Taasisi hiyo tayari ina Hakimiliki hivyo sio ruhusa
kwa mtu yeyote kuitumuia bila makubaliano na mmiliki.
“Natoa
wito kwa Wadau wa Sanaa kusajili kazi zao COSOTA ili watambulike na
kulindwa kisheria, pia waje kupata elimu ya haki za kazi zao ili kuepuka
migogoro isiyokua na ulazima” alisema Bw. Lyamuya.
Kwa
upande wake, Msanii Upendo Nkone ameishukuru COSOTA kwa kumsaidia
kupata haki katika kazi yake ambayo ilirudiwa bila raidhaa yake huku
akitoa wito kwa jamii kuacha kurudia kazi zake bila ridhaa yake kwakua
kazi zake zinalindwa kisheria kwakuwa amezisajili, na kwamba amewaasa
wasanii kujisajili BASATA na kusajili kazi zao COSOTA kwa sababu vyombo
hivyo vinawatetea wasanii.
Vile
vile Muandaaji katika Studio ya DOM –TUNE Bw. Kassim Ally amekiri
kufanya makosa hayo na kwamba ameahidi kuheshimu maridhiano yaliyofikiwa
huku huku akiishukuru COSOTA kwa kumueleza utaratibu unaopaswa kufuatwa
iwapo atahitaji kurudia kazi za msanii yeyote.
Kikao
hicho kimemalizika kwa maamuzi kwamba Studio ya DOM- TUNE ifute wimbo
wa msanii huyo katika mitandao ya kijamii na kulipa fidia ya kiasi cha
fedha walichokubaliana ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...