Na Leandra Gabriel, Dar es Salaam
MKUU wa Majeshi Tanzania CDF Venance Mabeyo amesema hadi sasa nchi na mipaka yake ni salama na wataendelea kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
CDF Mabeyo ameyasema hayo leo Machi 26 wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Joseph Magufuli Wilayani Chato mkoani Geita ambapo amesema kuwa kwa niaba ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini anahakikisha uimara wa ulinzi na usalama ambao pia utaendelea kuimarishwa.
"Tutaendelea kukulinda ukiwa Rais wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu na sio Amirati kama ilivyokuwa inapendekezwa, vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kukutii na kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.'' Amesema CDF Mabeyo.
Aidha Mabeyo amesema vyombo vya ulinzi vinamhakikishia Rais Samia uadilifu, utii na uaminifu kwa mujibu wa mila na desturi za majeshi katika kuhakikisha ulinzi na usalama kama ilivyokuwa katika awamu zote za uongozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...