Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Kikundi Cha Wanawake wenye Maono (Women with Vision) cha Mkoani Kagera kwa Kushirikiana na Wadau mbalimbali Nje na Ndani ya Mkoa huo, wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwakutanisha Wanawake Kuzungumza, na kuburudika pamoja katika Ukumbi wa Lina's Bukoba Manispaa Machi 08, 2021.

Mratibu Mkuu wa Tukio Hilo ambalo halikuwahi kufanyika tangu Sherehe hizi zimekuwepo Bi. Regina Zachwa akiongea na Michuzi TV amekaririwa akisema kuwa Tukio hilo ni kwa Mara ya kwanza kufanyika na kwa Mwaka huu wameamua kujikusanya Wanawake wenye mtazamo chanya kifikra na Kimaendeleo wakiwemo ambao tayari wamefanikiwa na ambao wapo katika nafasi tofauti, lengo ni kukutana na Wanawake wengine Mkoani Kagera kupeana mbinu za kuinuana kiuchumi na nyanja nyingine za kimaisha.

Aidha Regina ambaye ni mfanyabiashara na mwekezaji katika Redio Kasibante ya Mjini Bukoba ameongeza kuwa huo Ni mwanzo Wanakagera watarajie Mambo makubwa zaidi ambayo yatamuinua mwanamke. Shughuli hiyo ilipambwa na mada mbalimbali zilizowasilishwa,  huku Jukwaa likipambwa na Burudani nzuri ya Wasanii Lina Sanga, Isha Mashauzi na Live Band.

Bi. Regina Zachwa Mratibu wa Hafla ya Usiku wa Mwanamke akifurahi pamoja na Mama mwenye changamoto ya Viungo ambaye alifika ukumbini Lina's kuwakilisha akina mama wenye mahitaji Maalum.
Wafanyakazi pamoja na Malikia wa CRDB Bukoba, wakifurahi kwenye nembo yao wakiwa Ni miongoni mwa wadhamini waliofanikisha Usiku wa Mwanamke Kagera.
Mshereheshaji Shamila kutoka Kasibante Redio akiendelea kupangua matukio kwenye Ratiba ya Usiku wa Mwanamke
Isha mashauzi Msanii wa Taarabu Ni Kati ya Wasanii walioshusha Burudani murua ndani ya Lina's Bukoba katika Usiku wa Mwanamke
Lina Sanga Msanii wa Bongo Fleva akiingia Ukumbini Lina's Bukoba wakati wa Hafla ya Usiku wa Mwanamke
Sehemu ya Wageni na Waandaji wa Usiku wa Mwanamke Bukoba wakiendelea kufuatilia Matukio Ukumbini Lina's
Sehemu ya Wageni na Waandaji wa Usiku wa Mwanamke Bukoba wakiendelea kufuatilia Matukio Ukumbini Lina's
 Dansa kutoka Band ya Muziki ya Cassanova akionesha umahili wake wa minenguo ya kizaire

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...