Na,Jusline Marco:Arusha

Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TAHA Bi.Jacquelini Mkindi amesema kuwa wataendelea kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na hayati Dkt.John Magufuli katika sekta ya kilimo ikiwemo na ujenzi wa bandari na ipanuzi wa viwanja vya ndege nchini.

Mkindi amesema hayo wakati akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo amesema kupitia yote hayo wao wanayaona kwenye kilimo kama fursa ya kuwawezesha kuweza kuwekeza zaidi kwenye kilimo na katika kufanya biashara ndani na nje ya Tanzania.

"Sisi tutaendelea kumuenzi hayati Dkt.John Pombe Magufuli kwanza kama viongozi wa sekta binafsi kwa kuyaendeleza kwa vitendo na ufanisi mkubwa huku tukilinda heshima ya Tanzania lakini vilevile tukitumia kwa uangalifu na uadilifu mkubwa rasilimali tulizonazo."alisema Jacqueline

Aidha amesema kiu ya hayati Dkt.John Magufuli ilikuwa ni kuoana sekta ya kilimo inafanya maendeleo kwa kufanya kazi na kutumia vyema rasilimali ikiwemo miradi mbalimbali ambayo ameiacha ambapo wataendelea kufanya karibu na serikali ya Tanzania na kushirikiana na Rais wa awamu ya sita kwa hali na mali katika kuhakikisha yale ambayo hayati aliyaacha yanaendelea na wanaendelea kuyatekeleza kwa manufaa ya taifa na watanzania kwa ujumla.

Aliongeza kuwa katika uongozi wake hayati Dkt.Magufuli alizindua rasmi programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) ilitokuwa inaainisha maeneo ya vipaumbele katika kuendeleza sekta ya kilimo hapa nchini ambapo utekelezaji wake umeendelea kwa sehemu kubwa tangu mwaka 2018.

Bi.Jacqueline ameeleza kuwa baadhi ya mafanikio yalitopatikana katika kipindi cha uongozi wake ni pamoja na maboresho ya kisera yaliyopelekea ipatilanaji wa pembejeo na zana bora za kilimo kwa gharama nafuu.

"Tutamkumbuka pia nia yake ya dhati ha kuendeleza tasnia ya horticulture kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo ununuzi wa ndege ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya horticulture,kuongeza mkazo katika kuendeleza tasnia ya horticulture kutokana na ukuaji wake wa kasi hapa nchini.Alisema Jacqueline

Pamoja na hayo Bi.Jacqueline kwa niaba ya sekta ya kilimo na wanawake wote walio katika sekta ya kilimo Tanzania amempongeza Mhe.Samia Suluhu kwa kuteuliwa kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidi kuwa bega kwa bega na kusema kuwa watafanya kazi kwa karibu na kutekeleza yale ambayo wanatakiwa kuyatekeleza.


Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TAHA Bi.Jacqueline Mkindi akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...