Charles James, Michuzi TV

HATUONDOKI! Wananchi wa Jiji la Dodoma na viunga vyake ambao wamekosa nafasi ya kuingia kwenye uwanja wa Jamhuri kumuaga mpendwa wao aliyeku Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli wamekaa nje ya uwanja huo wakisubiri shughuli ya kuaga mwili huo iishe ndani na wao wapate kumuaga wakiwa nje.

Ndani ya uwanja wa Jamhuri umati wa wananchi waliojitokeza kumuaga Dk Magufuli ni mkubwa kiasi kwamba mageti yamefungwa ili kwa sababu za kiusalama na wananchi waliopo nje ya uwanja watapata fursa ya kumuaga kwani gari lenye mwili wake litapita kwenye barabara za jiji la Dodoma.

Shughuli za kutoa heshima ndani ya uwanja bado zinaendelea ambapo Marais wa Nchi mbalimbali barabarani Afrika na wale waliotumwa kuwawakilisha wakuu wao wa Nchi wanaendelea kutoa salam zao za rambirambi huku wengine wazielezea sifa za Dk Magufuli.

Nje ya uwanja wa Jamhuri zimefungwa 'screen' kubwa zikionesha shughuli yote ambayo inaendelea ndani ya uwanja huo ili wananchi waliokosa nafasi ya kuingia kuweza kushuhudia wakiwa nje.

Baadhi ya wakuu wa Nchi waliopo uwanjani hapa ni pamoja na Rais wa Kenya, Zambia, Zimbabwe, Malawi Msumbiji, Comoro, DR Congo, Afrika Kusini huku nchi kama Uganda, Rwanda na Burundi wakituma wawakilishi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...