Na Rahel Pallangyo, Dodoma
OMAR Abdulkadir amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa mpira wa miguu (Frat) uliofanyika leo jijini Dodoma.
Abdulkadir alipata kura 65 na kumshinda Joseph Mapunda aliyekuwa anatetea kwa kura 19.
Nafasi ya Mwenyekiti ililazimika kurudiwa baada ya Abdulkadir kutofikisha asilimia 51, awali Abdulkadir alipata kura 34 Mapunda kura 23 na Josephat Bulali aliambulia kura 19.
Makamu Mwenyekiti ni Emmanuel Chaula aliyepata kura 65 na kura nne zilimkataa.Katibu Mkuu ni Charles Ndagala aliyepata kura 57 akimshinda Israel Nkongo aliyepata kura 11 na mweka Hazina ni Rajabu Tambwe aliyepata kura 61.
Mwakilishi wanawake ni Isabela Kapela aliyepata kura 37 na kumshinda Marry Kapinga aliyepata kura 33.
Mkutano Mkuu wa TFF alichaguliwa Alanus Luena kwa kura 28, akiwashinda Damian Mabena kura 22 na Anthony Kayombo kura 14 na Kilingiri Bandoma aliyeambulia kura sita. Kamati ya Utendaji ya Frat waliochaguliwa ni Maulid Mwikalo kwa kura 67 na Jovin Ndimbo kwa kura 63.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...