Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
CHUO Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) kimesema kuwa wahitimu katika hicho ni wanaweza kufanya kazi popote pale duniani kutokana umahiri wa upikaji wa wataalam.
Wahitimu wa Chuo hicho 118 wamefanya mahafali kwa njia ya mtandao kwa baadhi kuingia katika ukumbi.
Akizungumza katika mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Aga Khan yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Joe Lugalla amesema kuwa Chuo hicho tangu kilipoanzishwa kimekuwa kinatoa katika fani ya elimu,udaktari bingwa pamoja na Uugugzi na ukunga na wanahitimu wamekuwa wakifaya vizuri katika sehemu zao za kazi.
Profesa Lugalla amesema katika udahili wanafanya kwa kuzingatia idadi ya walimu na sio kujaza wanafunzi katika madarasa.
Amesema kuwa wahitimu wanachotakiwa kufanya ni kusimamia taaluma zao sehemu za kazi na kuleta tija katika maendeleo ya nchi.
Kwa upande wa mkuu wa Chuo cha Udaktari Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania, Profesa Hussein Kidanto amesema katika uandaji wanafunzi wa ngazi ya uzamili wanafanya mafunzo katika Hospitali ya Aga Khan ambayo ina kila kitu.
Profesa Kidanto amesema kuwa wahitimu wameandaliwa na kwenda kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma katika Sekta ya afya.
Mhitimu wa ngazi ya Uuguzi Somoe Mohamed amesema kuwa anakwenda kubadili mtazamo wa wauguzi wa kutojali wagonjwa na kuwa sehemu ya wauguzi wanaojali wagonjwa.
Amesema mgonjwa akiangaliwa vizuri hata kama ana maumivu yanapungua kutokana na huduma ya muuguzi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...