Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MKONGWE katika Tasnia ya Uchekeshaji Mjuni maarufu Kama Mpoki ameondoa utata kwa Mashabiki wa Vengu.

Mpoki akizungumza katika kipindi cha redio ya EFM kipindi cha Joto la asubuhi amesema Vengu bado yupo hai anaendelea na shughuli zingine sio Sanaa kwa Sasa.

"Ilizuka minong'ono mingi wakati anaumwa badae wakazusha kuwa kafariki hapana ni uongo mtupu,kitu ambacho hawakifahamu kuhusu Vengu napenda kumuita Joseph Shamba yule ni mpole kundi zima."

Hata hivyo Mpoki amesema kutokuonekana karibu na Wasanii hao wanaounda kundi la 'Ze comedy' haimaniishi kuwa wametengana au kundi limevunjika kabisa.

"Tuna Mawasiliano mazuri karibia wasanii wote wa kundi letu na kwa Sasa Tumekua kila mtu kivyake vyake kutokana na majukumu pia Mimi nipo Redioni, Joti yuko na shughuli zingine hata hivyo Masanja ana harakati zake."

Mpoki amemtaja Mac Regan Kama Mchekeshaji bora kwake kwa muda wote.
"Jamaa anajua Sana na jinsi ya upekee wake na Sauti yake ile ya Shemeji ."

Mbali na Mafanikio aliyopata kupitia Sanaa ya Uchekeshaji Mpoki amesema ana Miliki nyumba 11 huku akiweka wazi changamoto alizopitia Hadi kupelekea kujiweka kwenye Mlolongo na Watu mbalimbali.

"Wakati naigiza Sauti ya aliyekua Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) pro.Lipumba wafuasi wake wakanitumia Ujumbe kuwa namdhihaki Kiongozi wao na niache Mara 1 kutumia Sauti hiyo ikanilazimu niandike barua ya kuomba radhi nashukuru walinielewa."

Vilevile Mpoki ameongezea kuwa kwa Sasa anapatika kwenye kipindi cha redio huku kazi zake za Sanaa zinaendelea Kama kawaida hajaacha Sanaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...