Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongo Flava nchini Heri Samir aka Mr Blue anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumsaka mlimbwende wa Miss Kahama ambalo limepangwa kufanyika Juni 5 mwaka huu katika ukumbi wa African Lounge ulioko Mjini Kahama.

Akizungumza na Michuzi TV, Mkurugenzi wa Kampuni Br. Black Social Partners ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Peter Frank amesema maandalizi ya kumpata Malkia wa Urembo Kahama yapo katika hatua za mwisho ambapo washiriki 12 wanatapanda jukwaani kumsaka mshindi.

Amesema mshindi wa Miss Kahama atapata nafasi ya kwenda kuwakilisha mji huo katika mashindano ya Miss Tanzania ambayo yatafanyika baadae mwaka huu.

Ameeleza kuwa wameandaa zawadi na fursa mbalimbali kwa washiriki wa Miss Kahama ambazo zitawasaidia katika maisha yao huku akitoa wito kwa wapenzi wa Urembo na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shindano hilo.

" Kumekuepo na sintofahamu mitandaoni kuhusu shindano hili la Miss Kahama lakini niwatoe hofu watu wa Kahama na wapenda burudani na urembo kwamba shindano lipo kama kawaida Juni 5 na mkali wa Bongo Flava, Mr Blue ndie atakayepamba shindano letu," Amesema Mwandaaji wa Shindano hilo Peter Frank.

Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania, Benard Mwata amesema wametoa baraka ya kufanyika kwa shindano hilo baada ya kuridhishwa na taratibu na maandalizi ambayo yamefanywa na waandaji wa Miss Kahama ambao ni Kampuni ya Br.Black Social Partners.

" Niwapongeze waandaji wa shindano hili la Miss Kahama kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa, hivyo Br.Black Social Partners chini ya Mkurugenzi wake Frank Peter ndio waandaji rasmi wa shindano hili ambalo litanyanyua vipaji vya mabinti wa Kahama," Amesema Mwata.

Ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa wadau wakubwa wa Urembo na kwamba anaamini warembo wote 12 watatumia jukwaa hilo la Miss Kahama kuonesha vipaji vyao katika jamii na kutanga utalii na uwekezaji katika Mji wa Kahama.

Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata akizungumzia shindano la Miss Kahama mwaka huu na upande wa  Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex ambaye ni Mwandaaji wa Shindano la Miss Kahama 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...