Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa nchini Zambia Clatous Chota Chama amepata pigo baada ya mkewe Mercy Munuka Chama kufariki dunia leo Mei 29,mwaka huu wa 2021.

Mkewe Chama amefariki nchin Zambia na tayari wadau mbalimbali wa soka katika nchi za Tanzania na Zambia zimetoa pole kwa Chama na familia yake kutokana na msiba huo.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Klabu ya soka ya Lusaka Dynamos Rabecca Mumba amesema bodi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo kwa  ujumla  wamesikitishwa na taarifa za kifo cha mkewe Chama.Mshanbuliaji huyo aliyewahi kuwa kiungo wa Klabu hiyo tayari yuko nchini humo kutokana na kupatwa na msiba huo mzito.

Mumba amesema Klabu ya Lusaka Dynamos inatoa pole kwa wafiwa sambamba na AIiyekuwa Nahodha wetu. Mioyo yetu ipo pamoja na Familia za wafiwa."Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu"

Hata hivyo hadi sasa bado haijawekwa wazi chanzo cha kifo cha mke wa Chama.Michuzi TV na Michuzi Blog itaendelea kukupa kila kinachoendelea kutokana na msiba huo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...