Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo na Maneja wa Kampuni ya CRJE East Afrika Ltd tawi la Tanzania Xu Cheng wakionyesha nyaraka za mkataba wa ujenzi Chuo cha Ufundi Dodoma  baada ya kutia saini. Ujenzi huo utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 17 na Chuo hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 5000.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo na Maneja wa Kampuni ya CRJE East Afrika Ltd tawi la Tanzania Xu Cheng wakionyesha nyaraka za mkataba wa ujenzi Chuo cha Ufundi Dodoma  baada ya kutia saini. Ujenzi huo utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 17 na Chuo hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 5000.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo na Maneja wa Kampuni ya CRJE East Afrika Ltd tawi la Tanzania Xu Cheng wakitia saini mkataba wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma katika hafla ya utiaji iliyofanyika Jijini Dodoma. Wanaoshuhudia katika picha ni watumishi wa wizara na Kampuni ya CRJE.


KUPITIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inajenga Chuo cha Ufundi katika Mkoa wa Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 5000 ili kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa ujuzi na maarifa.​

​Akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa chuo hicho uliofanyika Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema ujenzi wa chuo hicho utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 17 kupitia mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ) unaosimamiwa na Wizara.​

Katibu Mkuu huyo ameitaka kampuni iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa chuo hicho, CRJE East Africa Ltd. kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo ndani ya miezi 18 kama Mkataba unavyoonyesha.​

“Leo tumesaini mkataba wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma, ni matarajio yangu kitakamilika kwa wakati na​ubora unaotakiwa ili malengo ya kuanzishwa kwa chuo hiki yaweze kutimia,” amesema Dkt. Akwilapo.​

Naye Meneja wa kampuni ya CRJE East Africa Ltd. tawi la Tanzania, Xu Cheng ameahidi kutekeleza mradi huo​ kwa ubora unaokubalika na kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa.​

Mradi huo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya Jengo la Utawala, Ofisi za Idara, nyumba za watumishi, mabweni, Zahanati, Vyoo vya wanafunzi na watumishi, karakana tatu na kituo cha kupoza umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...