Hayo yameelezwa leo Mei, 20,2021 na Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo hapa nchini, Laetittia Willium wakati akitoa mada katika mkutano wa kujadili ubora wa viwango na usalama wa Mahindi hapa nchini, Mkutano uliofanyika, hoteli ya Serena Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa gharama hizo ni pamoja na za kutengeneza mifuko ya kinga njaa(Pics bargs)
Licha ya hilo ameomba Serikali kuwekeza kwenye tafiti ambazo zitatoa taarifa sahihi za kukabiliana na Sumu kuvu pamoja na kusambaza kwa wadau wa maeneo yote ya uzalishaji wa mahindi na Mazao ya mafuta.
Hata hivyo amesema kuwa wadau wengi zaidi wakihusishwa katika mikakati ya kukabiliana na sumu kuvu itafaa zaidi kutokomeza sumu hiyo ambayo inasababisha kushuka kwa gharama za mazao ya nafaka pamoja na mazao ya mafuta na mnyororo aa thamani wa mazao hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Usalama wa Chakula kutoka wizara ya kilimo, Honest Kessi amesema Serikali inampango kabambe wa kupambana na Sumu kuvu huku ikilinda afya ya walaji wa mwisho wa mazao ya nafaka na mazao ya mafuta na kuongeza wigo wa biashara.
Kessi ambaye alimwakilisha waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa serikali ina malengo madhubuti katika kutoa elimu ya kutokomeza sumu kungu ambayo inaharibu afya za walaji pamoja na kupunguza thamani ya mazao ya biashara yanayoshamuliwa na kuvu wakati wa kulima, shambani, wakati wa kuvunakutoka namna ya kuhifadhi pamoja na usafirishaji.
"Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano kumekuwa na uzalishaji wa mazao hususani zao la mahindi kwa mwaka 2020/2021 tumeshazalisha tani bilioni 6.7, ongezeko hili limeongeza fursa ya biashara ya mahindi katika soko la ndani na nje ya nchi, licha ya hilo biashara ya mahindi imekuwa na changamoto." Amesema Kessi
Amesema ni muhimu kujadiliana namna bora ya kuzuia sumu kuvu kuanzia uzalishaji wake mpaka uhifadhi wake kwani zao la mahindi ukiangalia katika mizania ya Chakula hapa nchini linachukua asilimia 36 kati ya mazao tisa ya mizania ya mazao tisa ya chakula kulingana na umuhimu wake katika afya za walaji.
Amesema kuwa majadiliano ya leo yalete majibu ambayo yatasaidia kuweza kuhifadhi mazao yetu kuaminika na yeyote atakayesema mahindi katika tuweze kujinasibu kusema kama unataka mahindi nenda Tanzania na sio nchi nyingine.
"Kwa umoja wetu tuliopo hapa kwa mawazo yetu na kwa nia yetu tutapata suluhisho la changamoto hii ya Sumu kuvu." Amesema Kessi
Hata hivyo Kessi amesema juhudi za Serikali kupitia wizara ya Kilimo ni kuna mpango wa kudhibiti sumu kuvu katika mazao ya nafaka pamoja na mazao ya mafuta.
Hata hivyo Serikali Kupitia wizara ya kilimo amesema kuwa inampango wa kueneza elimu ya kudhibiti sumu kuvu kuanzia kwa Mkulima, mhifadhi mazao, msafirishaji pamoja na walaji ili kutambua changamoto hiyo na kuiepuka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Godfrey Kirenga amesema kuwa Upatikanaji wa mahindi wa uhakika unasaidia kukua kwa uchumi wa Taifa pamoja na mtu mmoja mmoja kwani mataifa mengine watahitaji mahindi kutoka hapa nchini.
Hata hivyo Kirenga amesema kuwa uzalishaji wa mahindi unakuwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia hususani mbinu bora, mbolea, kufuata masharti ya mbegu bora pamoja na kuongeza eneo la uzalishaji.
Mkutano wa wadau wa kilimo hapa nchini wamekutana kujadili Changamoto ya Sumu Kuvu hapa nchini, kuangalia fursa za biashara ya mahindi katika soko la Afrika, Mipango ya serikali ya kupambana na sumu Kuvu, viwango vinavinavyopatikana vya mahindi na bidhaa pamoja na umhimu, uhitaji na upatikanaji wa Aflasafe.
Kongamano hilo lililokutanisha wadau mbalimbali wa kilimo limedhaminiwa na Sekta binafsi wakishirikiana na Serikali, Trade Mark East Afrika, banki ya NBC, banki ya NMB, benki ya CRDB na AGRA, wakishirikiana na SAGCOT, Kilimo Trust, AgroZ bya the Farmers Side, TBS, ACT, EAGC pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...