Na Richard Mwamakafu

 

CHAMA cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimeiomba Serikali kuingilia kati usimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho unataofanyika Juni, 26, mwaka huu ili haki itendeke.

 

Mwenyekiti wa TWFA, Bi. Amina Karuma   ametoa  ombi hilo leo  Mei, 26, 2021, Jijini Dodoma wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline  Gekul ofisini kwake.

 

Bi. Karuma amemwomba Mhe. Gekul kuuelekeza uongozi wa TFF na BMT kutoa ushirikiano kwa Chama hicho ili kufanya uchaguzi huru na haki kwa kuacha wanachama kumchagua Mwenyekiti wanayemtaka.

 

Aidha, Bi. Karuma amemwambia Mhe. Gekul kuwa TWFA kimepata mafanikio makubwa ambapo kiliweza kuanzisha Ligi Kuu ya Wanawake Nchini mwaka 2016 na pia kimewezesha kuandaa Timu ya Wanawake iliyoshinda mara mbili michuano ya kimataifa ikiwemo CECAFA na COSAFA.

 

Waziri Gekul amemuahidi kuwa, wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha  ili kukuza mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake hapa nchini ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la  kuinua mchezo huo hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...