Na Woinde Shizza , Michuzi Tv  ARUSHA

WAJASIRIAMALI  nchini wametakiwa kuzalisha bidhaa bora zenye tija na viwango hali ambayo itawasaidia kupata uhakika wa masoko ya ndani na nje ya nchi na kukabili ushindani wa  masoko duniani.

Mwenyekiti wa wakuu wa Taasisi za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya viwanda na biashara, Profesa Emanuel Mjema aliyasema hayo jana
alipokuwa akizungumza na wajasiriamali  wakati ujumbe huo
ulipofanya ziara katika ofisi za shirika la kuhudumia viwanda
vidogo(SIDO)Mkoani Arusha.

Ziara hiyo ambayo ilizikutanisha taasisi za serikali 15 zilizo chini
ya wizara hiyo ililenga kubadilishana uzoefu na ujuzi kati ya taasisi
hizo ikiwa ni pamoja na kutambua fursa za mawasiliano baina ya taasisi
husika ili waweze kuboresha huduma wanazotoa.

Profesa mjema ambaye ni Mkuu wa Chuo cha elimu ya biashara(CBE) mara
baada ya kutembelea kazi za wajasiriamali hao aliwapongeza kwa
shughuli walizozionyesha  ambapo aliwataka waongeze ubunifu ikiwa ni
pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana.

“Sisi CBE tumeendelea na tutazidi kuendelea kushirikiana na na wadau
wote ikiwa ni pamoja na nyie wajasiriamali na taasisi zingine za
Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa chuo chetu kinaongeza nafasi
za masomo ya biashara kwa wajasiriamali hapa nchini.”Alisisitiza
Profesa Mjema.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini(SIDO,) Sylvester Mpanduji alisema kuwa shirika lake litaendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali juu ya kuanzisha viwanda  pamoja na kuongeza ubora katika bidhaa zao.

“Wajasiriamali wengi tuliowatembelea walieleza matatizo mbalimbali yanayowakabi ikiwa ni pamoja na mitaji ,ucheleweshaji wa
vibali vya kuanzisha biashara zao na sisi tunawaahidi tutaendelea
kuwapatia mikopo kwani tumekuwa tukitoa mikopo hadi ya thamani ya
shilingi milioni tano”alisema Mpanduji

Awali Meneja wa SIDO Mkoani Arusha, Nina Nchimbi aliwataka wajasiriamali
kutoka maeneo mbalimbali mkoani hapo kufika katika ofisi za shirika
hilo ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa ikiwa ni
pamoja na mafunzo ya ujasiriamali.

Nchimbi alisema kuwa matatizo ambayo wamekuwa nayo wajasiriamali ni kutopata taarifa sahihi  zikiwemo za namna ya kupata mikopo ya
kukuza mitaji yao pamoja na kuzifikia taasisi mbalimbali za Serikali
kwa ajili ya kuisajili bidhaa zao na kwamba kupitia SIDO tatizo 
hilo itakuwa historia.

Katika ziara hiyo ujumbe huo ulitembelea viwanda mbali mbali vikiwemo vya zana za teknolojia(TDC),vya usindikaji unga lishe,bidhaa za
nyama,viwanda vya uchakataji vyuma,vifaa vya ujenzi ambapo
wajasiriamali mbalimbali walionesha bidhaa wanazozalisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...