Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini Dk. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya kilichotokea siku ya Juni 7,2021 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dk.Mzindakaya alikuwa Kiongozi Mwandamizi katika Chama Cha Mapinduzi na Serikali, ambae ametumikia katika nyadhifa mbalimbali kuanzia wakati wa TANU na baadae CCM akiwa mtumishi katika Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Katibu wa CCM Mkoa, Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
Taarifa ya CCM iliyotolewa leo Juni 8,2021 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka imesema "Chama Cha Mapinduzi kimempoteza Kiongozi mahiri, mchapakazi, mzalendo na mwenye msimamo usiyoyumba.
"Katika kupigania maslahi ya Taifa wakati wote wa utumishi wake ndani ya Chama na Serikali na hata baada ya kustaafu alikuwa na mchango mkubwa katika kulisaidiaTaifa,"imesema taarifa hiyo ambayo pia inaeleza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho.
Shaka amesema Chama Cha Mapinduzi kinatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na tunamuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na ustahimilivu katika kipindi.
"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu Dkt. Crisant Majiyatanga Mzindakaya mahali pema peponi.Sisi ni wa Mwenyezimungu na kwake tutarejea,,"amesema Shaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...