Na Mwandishi Wetu, Mtwara

WAFANYABIASHARA wa soko la Sabasaba manispaa ya Mtwara Mikindani wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti kwenda katika soko hilo na kusikiliza sababu zao ambazo zinawafanya waendelee kubaki katika soko hilo licha la agizo la mara kwa mara la viongozi wa mkoa kuwataka wahame.

Ombi hilo limekuja siku moja baada ya Mkuu huyo kuwataka wafanyabiashara hao kuhama mara moja kutoka katika soko hilo na kwenda katika soko jipya na la kisasa lilojengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 5.3.

Brigadia Jenerali Gaguti alisema jana kwamba wafanyabiashara hao wanapaswa kuhama kwa sababu haiwezekani serikali ikatumia fedha nyingi kujenga soko halafu lisitumie ipasavayo.

Hata hivyo wafanyabiashara hao ambao bado wapo katika soko hilo wamesema Mkuu huyo anapaswa kwenda na kuwasikiliza huku wakidai wanazo sababu zao za msingi ambazo wanapaswa kumueleza ili akazifanyie kazi katika kutekeleza agiza la kuwataka wahamie soko jipya la chuno.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao David Paul amesema kuwa wafanyabiashara hao wamewekeza na kujenga katika soko hilo na kwamba wana mikataba sababu ambazo zinawafanya washindwe kuondoka katika soko hilo.

“Sisi tuna mikataba hapa, tumewekeza hapa tumejenga hapa sio kwa msaada ya manispaa au wa serikali ni pesa zetu, lakini unaposema serikali imewekeza soko la Chuno mabilioni, lakini hata sisi tumewekeza hapa pesa zetu na mikata tunao,” amesema

Mwenyekiti huyo amesema kuwa na wao kupitia biashara zao katika soko hilo wanachangia kodi hivyo ni vizuri serikali ikatumia busara kwa kuwasikiliza kuliko kutumia nguvu kuwahamisha.

“Waangalie mikataba inasemaje sio watuhamishe tu kwa nguvu, serikali yetu ni sikivu itumie busara katika hili kwa kutusikiliza sisi pia kwa sababu tumewekeza pesa zetu hapa,” amesema.

Soko Jipya la Chuno lilipo Manispaa ya Mtwara Mikindani lilifunguliwa mwezi desimba mwaka 2020 na viongozi wa Mkoa kuwataka wafanyabiashara wa soko la sabasaba kuhamia katika soko hilo la kisasa.

Lakini baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kuwepo katika soko hilo la sabasaba licha ya maagizo ya mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa manispaa kuwataka wahamie soko la Chuno.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...