Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WADAU na watu mashuhuri nchini wametakiwa kuunga mkono ugawaji wa taulo za kike kwa wasichana wasiomudu gharama za taulo hizo na kwa wanafunzi wa kike waliopo mashuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Morogoro Kusini, Hamis Taletale 'Babu Tale' ambaye ameipongeza Taasisi ya Flaviana Matata iliyopo chini ya Mrembo Flaviana Matata kwa juhudi zake inazofanya za kugawa taulo hizo na kuhamasisha wadau wengine kuweka utaratibu wa kugawa taulo hizo kwa wenye uhitaji wakiwemo wanafunzi.
Tale amesema yapo maeneo mengine ambayo wanafunzi wa kike wamekua wakishuka kimasomo na wengine kuacha Shule kutokana na kushindwa kukosa taulo hizo pindi wanapokua kwenye siku zao za hedhi.
" Tumeshuhudia maeneo mengi mabinti zetu wakishuka kimasomo kutokana na wengi wao kukosa masomo kila mwezi kutokana na kushindwa kumudu gharama za taulo za kike pindi wanapokua kwenye mzunguko wao, ni jukumu letu kama Jamii na watu maarufu kuwasaidia mabinti hawa.
Nimpongeze Flaviana Matata kupitia taasisi yake kwa namna ambavyo wamekua mstari wa mbele kusaidia wasichana kupitia taulo zake za kike na hasa mabinti wa Jimbo langu la Morogoro Kusini, " Amesema Mbunge Tale.
Pamoja na ugawaji wa taulo hizo Tale ametoa wito kwa viongozi na wadau wengine kutoa elimu ya hedhi salama kwa wasichana mashuleni na jamii kwa ujumla.
Mbunge wa Morogoro Kusini, Hamis Taletale 'Babu Tale' akipokea taulo za kike kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Mrembo Flaviana Matata kwa ajili ya mabinti 56 wa Jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...