KAMPUNI ya TECNO mobile Tanzania imezindua simu mpya ya kisasa aina ya TECNO Phantom X yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zozote.

Simu hiyo yenye ukubwa wa GB 256 itamsaidia mtumiaji kuhifadhi data zake kwa urahisi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa simu kujaa. 

Meneja masoko wa TECNO Mobile Tanzania William Mota amesema simu hiyo ina Ram 8 ambayo inawezesha kufanya kazi kwa haraka zaidi na ni nzuri kwa matumizi mbalimbali katika kuhifadhi kazi zao pamoja na ukubwa wa kioo chake no Inch 6.7 kioo ambacho kitawasaidia wale wote wanaopenda kusoma kupitia simu kwa usahihi.

 Aidha Mota amewatoa hofu watumiaji wa simu hiyo kwa kueleza kuwa simu hiyo itakidhi mahitaji yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...