Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mfuko wa maendeleo ya jamii wa kunusuru Kaya maskini TASAF 111 awamu ya pili ,unatarajia kunufaisha Kaya Milioni 1.4 nchi nzima, kuwatoa walengwa wa mfuko huo kwenye umaskini.
Hayo yamebainishwa leo na Samsoni Kagwe kutoka TASAF makao makuu, wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa TASAF, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wawezeshaji ambao watakwenda kuratibu zoezi la kubaini Kaya Maskini katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Amesema mpango huo wa TASAF 111 awamu ya pili, utatekelezwa ndani ya miaka Minne, na ulianza rasmi 2020- 2023, ambao utanufaisha Kaya Milioni 1.4 sawa na wakazi Milioni 7, ambao wataondokana na umaskini.
"Mpango huu wa TASAF 111 awamu ya pili, utatekelezwa katika Halmashauri zote nchi nzima ikiwamo na Zanzibar, kwa kuziwesha Kaya Maskini kuinuka kiuchumi, na gharama za mpango huu kwa kipindi hiki ni Sh.Tirioni 2.03," amesema Kagwe.
"Mambo ambayo yatazingatiwa kwenye mpango huu, ili kuwatoa walengwa kwenye umaskini, ni kuongeza Rasilimali za uzalishaji mali, ikiwamo ufugaji wa mifugo, kilimo,uvuvi, na shughuli mbalimbali za kijasiriamali," ameongeza.
Pia ameongeza mambo mengine ambayo yatatekelezwa, ni kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi, ikiwamo upatikanaji wa huduma ya maji, afya, na elimu.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, amewataka waratibu ambao watakwenda kubaini Kaya hizo Maskini wilayani humo, wakalifanye zoezi hilo kwa uaminifu mkubwa, na kutoingiza Kaya zisizo kuwa na sifa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Boniphace Nchambi, amesisitiza zoezi hilo likafanyike kwa uaminifu mkubwa ili kusiwepo na Kaya hizo hewa.
Wawezeshaji wa kubaini Kaya Maskini Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa kuratibu zoezi la kubaini Kaya Maskini.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wawezeshaji wa kwenda kuratibu zoezi la kubaini Kaya Maskini wilayani humo.
Picha ya pamoja ikipigwa Mara baada ya mafunzo kuhitimishwa kwa siku ya kwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...