Madam Baby Baraka Chumaakizungumza na baadhi ya wananchi walio tembelea katika banda la RUCU katika maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
WADAU na wanafunzi wanaotaraji kujiunga na elimu ya juu wametakiwa kutembelea Banda la Chuo Kikuu Cha Ruaha ndani ya maonyesho ya vyuo vikuu vinavyoendelea mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Tv katika viwanja hivyo Madam Baby Baraka Chuma Amesema wanafunzi wakifika katika Banda hilo watakutana na fursa mbalimbali ikiwemo udahili wa moja kwa moja.

"Tunawaalika wanafunzi wote waje hapa kwani hapa tunafanya udahili wa moja kwa moja na kuwashauri wanafunzi juu ya masomo yao watakapokuwa chuoni na nini wafanye hili wapate michepuo sahizi." Amesema Madam Chuma.

Ametaja kuwa RUCU inatoa kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti mpaka shahada ya kwanza kwa fani mbalimbali.

Amesema kuwa wanafunzi wanaosoma RUCU wamekuwa Bora zaidi katika Maeneo mbalimbali ya kazi pindi wanapomaliza shule.

Ametolea mfano wa wanafunzi wa shahada ya Sheria na wale wanaosoma kozi ya Diploma ya Phamasia kutoka chuoni hapo.

Ametaja kuwa wanafunzi wa Sheria usoma kwa miaka minne Hali ambayo uwasaidia kufanya vizuri pindi wanapokwenda kwenye shule kuu ya Sheria.

Alitoa wito kwa wazazi na walimu kujiunga na Chuo Cha RUCU hili waweze kupata elimu Bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...