MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Yara Tanzania katika huduma za kidigitali kwa kuzindua program ya yaraConnect unaenda sambamba na jitihada za serikali ya awamu ya sita ya Samia Suluhu Hassani katika kuinua uchumi kupitia uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Aliyasema hayo jijini Arusha jana, wakati akizundua program hiyo akisema elimu hii inayopatikana kupitia program hii italeta mchango mkubwa katika kuboresha sekta ya kilimo na mnyororo wake wa thamani katika mkoa huo ambao kwa sehemu kubwa uchumi wake unaimarishwa na kilimo na ufugaji.

“Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza kampuni ya Yara katika kuendelea kubuni mbinu za kidigitali ili kujiweka karibu zaidi na wateja wenu na wakulima kwa ujuma, tunapoizindua program hii ni matumaini yetu kama serikali kwa wadsau wote watatumia App hii vizuri kwa malengo ya kupata ufanisi na maendeleo katika kilimo chetu hapa Arusha.

“Wakulima wakipata elimu ya kutosha wataongeza uzalishaji na kuingia katika kilimo biashara, tutajitosheleza kwa chakula na malighafi ya viwanda vya kuchakata mazao, halmashauri zitapata mapato ya kodi, hii itasaidia sana kukua kwa uchumi wa Arusha na kwa nchi yetu kwa ujumla.

“Serikali ya Mkoa wa Arusha ipo tayari wakati wowote kuwapokea na kuwasilikiza pindi mpatapo changaomoto zozote zitakazohitaji msaada. Natoa wito kwa makampuni mengine ya pembejeo za kilimo kuiga mfano wa Yara kwani wamekuwa mstari wa mbele katika ubunifu na ndia maana bidhaa zao ninapendwa sana na wakulima sio Arusha tu bali nchi nzima”, aliongeza Bwana Mongella.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo alisema Yara imekuwa mstari wa mbele katika kubuni mbinu sahihi za kilimo kwa kutumia njia za kidigitali.

“Ni matumaini yetu kwa wasambazaji wa mbolea yetu watakuwa mabalozi wazuri wa bidhaa ztu na kutumia fursa tulizowaletea kupitia program hii ili kujiongezea kipato na kukuza biashara zao na kwa upande mwingine kufanikisha maendeleo yatokanayo na uchumi utakanao na sekta ya kilimo”, aliongeza mkurugenzi huyo.

Naye Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei alisema sasa wakulima wa mazao mbalimbali mkoani Arusha wanaweza kuwa na uhakika wa kupata matokeo bora ya kilimo wakifanyacho kutokana na taarifa za kitaalamu zinazopatikana katika program mpya ya yaraConnect iliyozinduliwa mkoani humo.

Meneja huyo alisema taarifa hizo zimewekwa katika eneo lionaitwa ‘video za maarifa zinazopatikana katika program hiyo ambapo kunapatikana taarifa zote za msimu wa ama iwe ni kupanda, kuvuna na taarifa nyinginezo muhimu za mazao yanayopatikana katika eneo husika.

“YaraConnect ina manufaa kwa wote, kwa wauzaji wa mbolea ya yara na kwa wakulima kwani sasa mkulima atakuwa na uhakika akienda kununua mbolea kwa muuzaji aliyejisajili katika program yetu atapata pia majibu ya maswali ya majibu ya changamoto zinazotokea shambani,” alisema Bwana Deodath.

Aidha alisema licha ya manufaa ya elimu ya utaalamu wa kilimo, wauzaji wa rejareja wa mbolea wa yara watapata faida nyingine kwa kujikusanyia pointi mara wafanyapo mauzo ya mbolea hivyo hivyo kujizolea zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja, pikipiki, pesa taslimu na zawadi nyinginezo.

Huu ni mkoa wa pili sasa kwa Kampuni ya Yara kuzindua programu hii ambapo mwanzoni mwa wiki uzinduzi huu ulifanyika mkoani Kilimanjaro huku uzinduzi huu ukipangwa kufanyika kwa mikoa saba nchini kwa lengo pia la kukutana na wauzaji wa mbolea ya yara na wadau wa sekta ya kilimoa kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kusikia changamoto zao ili kuona namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella (wa pili kushoto) akizungumza na wauzaji pamoja na wadau wa mbolea ya Yara jijini Arusha jana wakati wa Uzinduzi wa programu ya yaraConnect inayowezesha upatikanaji wa elimu ya utaalamu wa kilimo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo, Bwanashamba Mwandamizi wa kampuni hiyo, Maulidi Mkima na Afisa Kilimo mkoa wa Arusha, Daniel Loiruck.

Afisa Kilimo mkoa wa Arusha, Daniel Loiruck (kulia) akizungumza na wauzaji pamoja na wadau wa mbolea ya Yara jijini Arusha jana wakati wa Uzinduzi wa programu ya yaraConnect inayowezesha upatikanaji wa elimu ya utaalamu wa kilimo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella na Bwanashamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima.
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania,Deodath Mtei (kulia) akizungumza na wauzaji pamoja na wadau wa mbolea ya Yara jijini Arusha jana wakati wa Uzinduzi wa programu ya yaraConnect inayowezesha upatikanaji wa elimu ya utaalamu wa kilimo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo, Bwanashamba Mwandamizi wa kampuni hiyo, Maulidi Mkima na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella Mara baada ya uzinduzi Uzinduzi wa programu ya yaraConnect inayowezesha upatikanaji wa elimu ya utaalamu wa kilimo kwa wauzaji na wadau wambolea ya Yara. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Arusha jana. Kulia ni Bwanashamba Mwandamizi wa kampuni hiyo, Maulidi Mkima.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella (katikati) waliokaa, akipiga picha ya kumbukumbu na maofisa wa Yara Tanzania, wakala wao na waalikwa wengine mara baada ya uzinduzi huo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...