Na Mwamvua Mwinyi,Mwanabwito
MKAZI
wa Kitongoji cha kazi Mwanabwito Kata ya Kikongo Halmashauri ya Kibaha
(Kibaha Vijijini) Mkoa wa Pwani Ramadhani amenusurika kuuawa kwa mkuki
na wafugaji jamii ya Wasukuma.
Tukio
hilo limetokea baada ya mmoja wa wakulima kuwakataza wasiingize mifugo
kwenye shamba la jirani yake, ambapo walipokatazwa kabla ya tukio hilo
walimjeruhi mkulima kwa kumpiga kwa fimbo kisogoni na mkononi ambapo
hali iliyosababisha mkulima huyo kushonwa.
Akizungumza
mbele ya Waandishi mkazi huyo alisema kuwa wakulima walikuwa wanane
wafugaji sita kabla ya kuitana na kuwa wengi zaidi ambao walimfukuza
wakiwa na mikuki, lakini aliwahi kujificha kwenye mabua yanayoota
kandokando ya mto Ruvu ndio ikawa salama yake.
"Walinikimbiza
umbali zaidi ya kilometa meta na ushehe, wenzangu walikuwa juu ng'ambo
ya mto wakiniita simu niliweka mtetemo ili isisikike, nilikaa kwenye
mabua hayo kwa zaidi ya dakika saba walipoona kimya wakajua nilishavuka
mto, wakageuka na kurejea kuchukua ng'ombe wao," alisema Pwimwilu.
Mkazi
aliyejeruhiwa akijitambulisha kwa jina la Yohana Mrope alisema kuwa
aliona makundi ya ng'ombe ikiingia katika shamba la jirani yake
alipokwenda kumsaidia alishtukia amepigwa fimbo ya kisogoni na mkononi
hali iliyomsababishia ashonwe na kwamba ana RB wanawatafuta
waliomshambulia na kuongeza kwamba anawatambua.
Nao
wakulima waluojitambulisha kwa majina ya Ashura Asha Kawa na Taison
Taison walisema kuwa hali ni mbaya kwani mifugo imekuwa kero kubwa kiasi
cha kuwavunja nguvu wakulima, huku wakiiomba serikali iwasaidie
kuondokanaa na changamoto hiyo waliyoielezea kuwa ni ya muda mrefu.
Mwenyekiti
wa Kitongoji hicho Juma Tupa alithibitisha kuwepo kwa kero hiyo, na
kwamba wamefika kwenye ofisi zote pasipo mategemeo hivyo tegemeo la
pekee kwa Rais Mama Samia Suluhu.
"Hili
suala la kero ya mifugo katika Kitongoji changu imekuwa kero kubwa
wananchi wangu wanashibdwa kulima kwa kuhofia mifugo, unapolima ujue
umejipalilia makaa hautokuwa na muda wa kufanya shughuli yeyote ya
maendeleo, kuanzia asubuhi mpaka jioni kazi yako kulinda ng'ombe mpaka
unavuna," alisema Singa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...