Na Mwamvua Mwinyi,Miono
WAKAZI
wa Kijiji cha Machala Kata ya Miono, Halmashauri ya Chalinze wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kupuuza uzushi unaosambazwa
mitandaoni na baadhi ya watu kuhusiana na chanjo ya CORONA, kuwa ina
madhara.
Aidha wametakiwa
kuungana mkono juhudi za rais Samia Suluhu alizozianzisha kuhusiana na
chanjo ya ugonjwa huo hatari, huku rais akiongoza zoezi hilo mpango
unaoendelea katika mikoa mbalimbali, huku serikali ikisisitiza kuwa ni
zoezi la hiyari.
Hayo
yamebainishwa na Mjasiriamali Maarufu wilayani hapa Teddy Davis,
alipozungumza kwenye mahafali ya shule ya msingi ya Machala iliyopo
kijiji cha Machala, akiwa mgeni rasmi ambapo alisema wayapuuze maneni
yanayozungumzwa mitandaoni.
"Nitumie
fursa hii kuwakumbusha kwamba hivi sasa dunia inaangaika kupambana na
ugonjwa hatari wa CORONA, niwaombe wa-Tanzania wenzangu tuungane na rais
wetu Samia Suluhu aliyeonesha kuguswa na janga hilo," alisema Mlezi
huyo.
Katika kupambana na
hali hiyo Teddy ameahidi kuwashoneshea barakoa wanafunzi wote pamoja na
walimu ikiwa ni kuungana na juhudi za serikali katika mapambano hayo,
huku akiahidi kupunguza changamoto zinazoikabili shule ikiwemo uchache
wa matundu ya vyoo.
Taarifa
ya Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Gao Rodgers imeelezea
mafanikio kadhaa pamoja na changamoto ya upungufu wa vyumba vitatu vya
madarasa, ofisi ya walimu sanjali na matundu ya vyoo.
Taarifa ya wahitimu hao 13 iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali ni
Mahafali
ya tisa tangu kuanzishwa mwaka 2007 ambayo imeelezea mafanikio na
changamoto kadhaa huku ikisisitiza upatikanaji wa vyumba vipya vitatu
vya madarasa, matundu ya vyoo na ofisi ya walimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...