Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula
asitisha makampuni matatu yaliyokuwa yakifanya urasimishaji makazi
katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kwa kushindwa kukamilisha kazi kwa
wakati.
Naibu
Waziri wa Ardhi alisema hayo wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati
akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya
hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika wilaya za mkoa wa
Dodoma.
Aidha,
ameagiza ofisi ya ardhi mkoa kukaa na mkurugenzi wa halmashauri ya Bahi
iundwe na timu ya mkoa ije hapa kwa gharama ya mkurugenzi ili
kukamilisha upimaji.
Naye
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Thadei Kabonge amesema
Kumeibuka tabia kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutojitokeza kuchukua
hati zao za umiliki wa ardhi kwa wakati kwa kigezo cha kukwepa kulipa
kodi ya pango ardhi kitu ambacho kwa sasa Bunge limeipatia muarubaini
tabia hii.
Kabonge ameongeza kuwa mwaka jana Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sharia kwamba ardhi ikishapimwa na ikapita miezi mitatu na mmiliki hajajitokeza kuja kumilikishwa basi itahesabika tayari ushamilikishwa na itaanza kuhesabiwa kodi ya ardhi.
Aidha, Kabonge wametakiwa wananchi kujitokeza ili kumilikishwa Ardhi kisheria kwa kukwa kutomilikishwa ardhi sio kigezo cha kukwepa kulipa kodi ya ardhi hata kama ardhi hiyo itakuja kumikishwa baada ya miaka kupita.
Kamishna Kabonge amebainisha kuwa ofisi yake ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma ina viwanja zaidi ya 2,550 ambavyo vimepimwa tayari lakini wananchi hawataki kumilikishwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...