MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) imeiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa hiari ili kukoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua pamoja na kuondoa changamoto ya kutegemea wanafunzi wa shule za sekondari katika uchangiaji damu.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Taifa ya Ukusanyaji Damu iliyoanza Septemba 20 (juzi), Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Avelina Mgasa amesema kauli mbiu ya kampeni za mwaka huu ni ‘Changia Damu Kuokoa Wanaoleta Uhai Duniani’.
Dk. Mgasa amesema hivi sasa wanaweka mkazo kwa jamii kujitolea damu kwa hiari kwani Mpango wa Taifa wa Damu Salama haujaweza kufikia lengo la kukusanya chupa za damu zinazokithi mahitaji ya nchi.
Amesema ripoti ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama imeonesha kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 kwa kushirikiana na timu za halmashauri wameweza kukusanya chupa za damu 312,714 zilikusanywa ambazo ni sawa na asilimia 57 ya mahitaji.
Dk. Mgasa amesema shirika la afya Dunniani (WHO) linaelekeza kila nchi mwanachama kukusanya damu asilimia moja ya wakazi wake au chupa 10 kwa kila wananchi 1,000 ili kujitosheleza na mahitaji ya damu salama wakati wote.
Amesema kwa takwimu za mwaka 2019/2020 Tanzania tumefikia chupa 6 kwa kila wananchi 1,000.
Akizungumzia changamoto za kupata wachangiaji wa damu, amezitaja kuwa ni pamoja na wanafunzi wanaosoma na hata wanaomaliza shule za sekondari kuwa na umri mdogo kwani sheria inawataka watu wenye umri wa miaka 18 hadi 65.
“Asilimia 80 ya damu inayokusanywa nchini inakusanywa kutoka kwa wannafunzi na vijana wanapokuwa shule za sekondari na vyuoni ambao wanamaliza wakiwa na umri mdogo hivyo hawapati fursa ya kuchangia damu wakiwa shuleni na wakirudi kwenye jamii huacha kuchangia,” amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...