Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi ndani yake Mbowe anashtakiwa pamoja na wenzake watatu.
Julai 30, 2021 Mbowe alifungua kesi hiyo ya Kikatiba namba 21 katika Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) akipinga utaratibu uliotumika katika kumkamata, kumuweka chini ya ulinzi na kumfungulia mashtaka.
Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 23, 2021 na Jaji John Mgeta aliyekuwa akisikilza shauri hilo.
Akitoa uamuzi huo Jaji Mgeta amesema, amepiti hoja za kimaandishi za pande zote mbili na ametupilia mbali hoja tatu zilizotolewa katika mapingamizi hayo huku akikubaliana na hoja moja ambayo ndiyo ilisababisha kufutwa kwa kesi hiyo.
Katika hoja hiyo ya kwanza upande wa wajibu maombi (Jamuhuri) walidai kuwa maombi ya Mbowe yalikuwa na kasoro na yako kinyume na kifungu cha 4(5) na 8(2) cha Sheria ya Haki za Msingi na utekelezaji wa majukumu kwa sababu mtoa maombi anazo njia nyingine za kupata hayo anayoyataka.
"Ni kweli Mbowe aliomba tamko la mahakama iseme kuwa ninm kweli haki zake za kikatiba zilivunjwa lakini kutokana na majibizano hayo, na vifungu vya sheria pamoja na kesi zilizotolewa kama kumbukumbu, na ukweli kuwa tayari kuna kesi nyingine ya msingi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na ufisadi aliona kwamba kesi hiyo haipaswi kuendelea katika mahakama hiyo. amesema Jaji Mgeta.
Amesema, kwa kuwa sasa hivi kuna kesi nyingine inayomkabili Mbowe katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, basi anaweza kutumia mahakama hiyo kutoa malalamiko yake na kupatiwa ufumbuzi, " Najikuta kwamba mahakama hii haina mamlaka ya kuendesha shauri hili hivyo maombi haya nayafuta." amesema Jaji Mgeta.
Hata hivyo hoja zilizotupwa katika mapingamizi ya awali yalitolewa na Jamuhuru ni pamoja na ile iliyodai kuwa maombi hayo yalikuwa ni upuuzi na kuongeza chumvi na pia yana kasoro kwa kuwa kuna mtu muhimu ambaye hakujumuishwa katika keshi hiyo.
Katika maelezo ya mapingamizi yao upande wa Jamuhuri ulidai kuwa maombi ya Mbowe yalitaja Mahakama ya Kisutu hivyo haikuwa sawa kuacha kujumuisha Mahakama ya Kisutu pamoja na Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi katika mahakama hiyo kabla ya kuhamishiwa Mahakama ya 'Mafisadi' hoja ambayo Jaji mgeta hakukubaliana nayo akieleza kuwa Mahakama hiyo pamoja na Hakimu huyo walikuwa katika utelezaji wa majukumu na utekelezaji wa haki na sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...