Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC,) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Lady Fatima Kigamboni jijini Dar es Saalam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja Uhusiano kutoka NIC Karimu Meshack amesema sera ya shirika hilo ni kurudisha kwa jamii kwa faida wanayoipata na hiyo ni pamoja na kusaidia miradi ya Serikali inayogusa jamii moja kwa moja hasa watoto, wanawake na wazee.
Karimu amesema, baada ya kuona uhitaji wa chakula katika kituo hicho wakaona ni vyema kuungana na kituo hicho kinacholea watoto yatima wapatao 25.
"NIC daima tupo karibu na jamii, na leo tumekuja kuwatembelea watoto wetu na kuwaletea mahitaji yatakayosaidia katika ukuaji wa watoto hawa...Tumeleta mahitaji mbalimbali ikiwemo unga wa sembe na ngano, mchele, maharage na mafuta ya kupikia." Amesema.
Aidha amesema, Shirika hilo lipo pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo afya na elimu zinawafikia wananchi.
Kwa upande wake mwanzilishi wa kituo hicho Omary Kalekela ameishukuru NIC kwa kuwatembelea na kutoa msaada wa vyakula kwa watoto hao na kuwakaribisha wadau wengine kufuata nyayo za NIC katika kushiriki kuwalea watoto hao kwa namna mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...